Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:49

Ukosefu wa chakula wahofiwa kuigubika Sudan - Mercy Corps


Wakimbizi wa Sudan wanaendelea kukimbilia Chad.
Wakimbizi wa Sudan wanaendelea kukimbilia Chad.

Ukosefu mkubwa wa chakula unahofiwa kutokea Sudan, iwapo mapigano yataendelea.

Haya ni kulingana na kiongozi wa shirika la kutoa msaada la Mercy Corps Freydoum Borhani, aliye kwenye jimbo la Gedaref, karibu na Ethiopia.

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha dharura cha RSF yanaingia mwezi wa tatu na hali ya kibinadamu inaendelea kuwa mbaya hasa katika mji mkuu wa Khartoum na sehemu zingine za nchi ikiwemo Darfur, ambapo mapigano yanaendelea.

Rais wa Kenya William Ruto alisema kwamba pamoja na viongozi wengine wa jumuiya ya Afrika mashariki, wanapanga kukutana na majenerali wa Sudan moja kwa moja, wiki ijayo, kujadili namna ya kumaliza vita hivyo.

Matamshi ya Ruto yanatolewa baada ya viongozi wa IGAD waliokutana Djibouti, kumteua Ruto kuwa mpatanishi katika mzozo wa Sudan lakini kiongozi wa Jeshi la Sudan amekataa uteuzi huo na badala yake anataka rais wa Sudan kusini Salva Kiir kuwa mpatanishi.

Zaidi ya wtu milioni 1.6 wmekoseshwa makao nchini Sudan, huku nusu milioni wakikimbilia nchi Jirani kutokana na vit hivyo.

Forum

XS
SM
MD
LG