Kabla ya hapo kulifanyika mapigano na mashambulizi ya anga usiku kucha, wakaazi walisema.
Jeshi la Sudan na kikosi cha dharura cha RSF wamekubaliana kujiepusha na mashambulizi na kutafuta maslahi ya kisiasa katika kipindi cha usitishaji mapigano, kilichoanza saa kumi na mbili asubihi, pamoja na kuruhusu kuwasilishwa kwa misaada, wapatanishi wa Saudia na Marekani wamesema.
Makubaliano kadhaa ya amani ya awali yameshindwa kusitisha mapigano.
Mgogoro wa kugombea madaraka kati ya pande hizo mbili umegeuza mji mkuu kuwa eneo la vita lililokumbwa na uporaji, na kusababisha milipuko ya mapigano katika maeneo mengine, na kuongeza kasi ghasia Darfur magharibi mwa Sudan.
Saa chache kabla ya kipindi cha kusitisha mapigano kuanza, mashuhuda waliripoti mapigano na mashambulizi ya anga katika maeneo kadhaa ya Khartoum na Omdurman, miji miwili inayopakana na kuunda mji mkuu inyotengenishwa na mto Nile.
Forum