Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 16:09

UNHCR imeahidi kuwapatia makazi maelfu ya wakimbizi walioko Malawi


Wakimbizi kutoka Rwanda wakicheza ngoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani katika Kambi ya Wakimbizi ya Dzaleka nchini Malawi tarehe 20 Juni, 2018. Picha na Amos Gumulira / AFP.
Wakimbizi kutoka Rwanda wakicheza ngoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani katika Kambi ya Wakimbizi ya Dzaleka nchini Malawi tarehe 20 Juni, 2018. Picha na Amos Gumulira / AFP.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi limeahidi msaada wake wa kuwapatia makazi mengine zaidi ya wakimbizi 50,000 na watu wanaoomba hifadhi nchini Malawi ambao hivi sasa wanaishi kwenye kambi ya Dzaleka yenye msongamano mkubwa katikati mwa nchi hiyo.

Hivi karibuni, serikali ya Malawi ilitangaza kuwa imepata eneo jipya kaskazini mwa nchi ili kusaidia kupunguza idadi ya wakimbizi katika kambi ya Dzaleka, ambayo awali ilifunguliwa kwa lengo la kuhifadhi takriban watu 12,000.

Mkurugenzi wa Kanda wa UNHCR kwa Kusini mwa Afrika, ValentinTapsoba aliahidi msaada wa uhamishaji baada ya mkutano na Rais wa Malawi Lazarus Chakwera, katika mji mkuu Lilongwe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo, Tapsoba alisema UNHCR imefurahishwa na nia ya dhati ya serikali ya Malawi kuboresha hali ya maisha na ustawi kwa jumla wa wakimbizi wanaoishi nchini humo kwa kuwapatia makazi mazuri zaidi.

Malawi iliifungua kambi ya Dzaleka mwaka 1994 ili kuwahudumia kiasi cha watu 12,000 lakini hivi sasa ni mwenyeji wa zaidi ya wakimbizi 50,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Rwanda, Burundi, Somalia na Ethiopia.

Kenyi Emmanuel Lukajo ni afisa wa mahusiano ya kigeni na habati kwa UNHCR nchini Malawi, anasema serikali itahamisha takriban wakimbizi 8,000, ambao wamekuwa wakiishi nje ya kambi, na tayari rasilimali ziko chache sana katika kambi.

“Maish ni magumu sana. Hakuna maji ya kutosha, hakuna makazi ya kutosha hata watoto ambao wanatolewa shule mjini hawana uwezo wa kuandikishwa shule kwasababu hakuna nafasi za kutosha. Kila kitu hakuna huko, kwahiyo fedha za kuwapatia watu wa ziada ambao wamehamishwa."

Wakimbizi wakifua nguo zao katika kambi ya Dzaleka. Picha na Amos Gumulira / AFP.
Wakimbizi wakifua nguo zao katika kambi ya Dzaleka. Picha na Amos Gumulira / AFP.

Malawi ilianza kuwahamisha kwa nguvu wakimbizi, ambao walikuwa wakiishi kinyume cha sheria kote katika maeneo ya vijijini na mijini nchini humo mwezi Mei, baada ya tarehe ya mwisho ya April 15 iliyowekwa na serikali ya kuondoka na kuhamia kwingine kwa hitari kufikia mwisho wake.

Katika taarifa yake, UNHCR inasema mpaka hivi leo, takriban watu 1,900 wamerejea kwenye kambi yenye msongamano ya Dzaleka huku kukiwa na changamoto za kifedha ambazo shirika hilo inakabiliana nazo katika kuwahudumia wakimbizi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linasema kuanzia Juni 1, limepokea asilimia 15 tu ya fedha ambazo walikuwa wakihitaji yaani dola milioni 27.2 kwa ajili ya wakimbizi na waomba hifadhi nchini Malawi mwaka huu.

Hata hivyo, serikali ya Malawi inasema imepata ardhi kwa ajili ya makazi mapya ya wakimbizi katika wilaya ya Chitipa, kaskazini mwa Malawi, ili kusuluhishoa matatizo ya msongamano wa wakimbizi.

Mkimbizi akipita njia ndani ya kambi ya wakimbizi ya Dzaleka. Picha na Amos Gumulira / AFP.
Mkimbizi akipita njia ndani ya kambi ya wakimbizi ya Dzaleka. Picha na Amos Gumulira / AFP.

Ken Zikhale Ng’oma ni waziri wa usalama wa ndani nchini Malawi. Aliuambia mkutano wa wana habari wiki iliyopita kwamba makazi mapya yatasaidia kuwafukuza wahalifu ambao wanaingia nchini Malawi kwa kisingizio cha kwamba ni wakimbizi na waomba hifadhi.

Ng’oma anasema “ndiyo maana tunataka kubadili mfumo wetu hivi sasa, wakati wowote tutaifunga kambi ya Dzaleka. Tatafungua kambi mpya huko Chitipa ambako tunataka kuhakikisha kwamba mtu yeyote ambaye anaingia Malawi ni vyema aangaliwe vyema kabla ya kuingia nchini kama wanavyofanya wamarekani. Hakuna anayetaka kuomba hifadhi ataambiwa ingia na ‘utume maombi ukiwa ndani’ hapana. Yote yatafanyika kwenye kituo cha kuingilia. Kwahiyo tunataka kuutumia mfumo wa Marekani.”

UNHCR inasema iko tayari kutoa msaada muhimu kwa ajili ya eneo jipya. “Kama serikali inasema wamepata eneo jipya, UNHCR haina pingamizi kwa hilo ilimradi UNHCR inahusishwa katika mchakato na halafu tunatathmini eneo hilo kuhakikisha kwamba eneo lina maji ya kutosha, haliko sehemi inayoweza kukumbwana mafuriko na eneo haliko karibu na mpakani. Kwahiyo masharti yote yatatekelezwa, basi UNHCR haitasita kusaidia katika mchakato.”

Maafisa wa serikali ya Malawi wamehakikisha kuhusika kwa UNHCR katika tathmini ya mchakato wa eneo na kushirikiana katika kupata rasilimali kwa ajili ya amendeleo ya makazi mapya.

Forum

XS
SM
MD
LG