Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 16:22

Watu zaidi ya laki moja kutoka Sudan wamekatisha mpaka kuingia Chad


Mfano wa wa-Sudan wanaokatisha mpaka kuingia Chad. May 3, 2023.
Mfano wa wa-Sudan wanaokatisha mpaka kuingia Chad. May 3, 2023.

Zaidi ya watu 100,000 wamekatisha mpaka na kuingia Chad tangu kuzuka kwa mzozo nchini Sudan mwezi Aprili, na idadi inaweza kuongezeka maradufu katika kipindi cha miezi mitatu ijayo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limeonya mapema mwezi huu

Maelfu ya wakimbizi wa Sudan waliokimbilia Chad kuepuka mapigano nchini mwao huenda wasipate misaada ya kibinadamu na matibabu wakati wa msimu wa mvua unaokaribia, shirika la misaada ya matibabu la Medecins Sans Frontieres (MSF) limesema Jumatatu.

Zaidi ya watu 100,000 wamekatisha mpaka na kuingia Chad tangu kuzuka kwa mzozo nchini Sudan mwezi Aprili, na idadi inaweza kuongezeka maradufu katika kipindi cha miezi mitatu ijayo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limeonya mapema mwezi huu.

Mkuu wa ujumbe wa MSF nchini Chad, Audrey van der Schoot, amesema mafuriko ambayo kwa kawaida hutokea katika kipindi hiki cha mwaka yanaweza kuwatenga wakimbizi na jamii zinazowahifadhi katika mkoa wa Sila mashariki mwa Chad na maeneo mengine ambayo yanapakana na Sudan.

Mvua pia zitaleta hatari kubwa ya magonjwa ya kuambukiza, kutokana na upatikanaji duni wa maji safi pamoja na usafi wa mazingira, alisema. Karibu wakimbizi 30,000 wako Sila, mahala ambako hawana makazi, maji na chakula kutokana na upungufu wa misaada ya kibinadamu. Wengi wamehamia huko wakifadhiliwa na familia za wenyeji, na kuweka shinikizo kwa rasilimali ndogo iliyopo, MSF ilisema.

Forum

XS
SM
MD
LG