Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:34

Wakaazi mjini Khartoum nchini Sudan hawajasikia milio ya risasi kwa saa 72


Wakaazi wa Sudan wanasema hawajasikili milio ya risasi na milipuko mingine tangu Jumapili asubuhi
Wakaazi wa Sudan wanasema hawajasikili milio ya risasi na milipuko mingine tangu Jumapili asubuhi

Utulivu ulio na tahadhari umeshuhudiwa mjini Khartoum siku ya Jumatatu, siku moja baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano ya saa 72 kuanza kutekelezwa. Utulivu huo ulitoa matumaini kwa raia wengi katika mji huo baada ya wimbi la ghasia za hivi karibuni.

Baadhi ya wakaazi wa mji mkuu wa Sudan, Khartoum, wanasema hawajasikia milio yoyote ya risasi tangu kuanza kwa usitishaji mapigano kwa saa 72 hapo Jumapili asubuhi. Wakaazi wanasema licha ya kwamba makubaliano hayo ya kusitisha mapigano yanaonekana yamezuiliwa lakini bado wana wasiwasi kuhusu uhaba wa bidhaa za msingi katika masoko ya ndani.

Utulivu ulio na tahadhari umeshuhudiwa mjini Khartoum siku ya Jumatatu, siku moja baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano ya saa 72 kuanza kutekelezwa. Utulivu huo ulitoa matumaini kwa raia wengi katika mji huo baada ya wimbi la ghasia za hivi karibuni.

Baadhi ya wakaazi wa mji mkuu Khartoum na eneo la El Obeid katika jimbo la Kordofan Kaskazini wanasema makubaliano hayo yanaonekana kuwa yanatekelezwa.

Akizungumza na VOA siku ya Jumatatu kutoka kitongoji cha Omdurman mjini Khartoum, Tariq Abdallah anasema hajasikia milio ya risasi wala makombora mazito kwa saa kadhaa.

Abdallah anasema ingawa pande hizo mbili zinazohasimiana zinaonekana kufuatilia usitishaji mapigano kwa wakati huu, lakini unyanyasaji na vitisho vya raia katika vituo vya ukaguzi, na ndani ya maeneo ya makazi vinaendelea kufanyika.

Mashine za vita zimesitishwa zaidi mjini Khartoum, pande hizo mbili zinazingatia makubalianoa ya usitishaji mapigano, zimeacha kupigana. Lakini vitendo vya ukatili dhidi ya raia havijawahi kukomeshwa.

Abdallah anabainisha kwamba wakati raia wakiendelea kuwa na matumaini ya mapigano kusitishwa, lakini bado hali ni ngumu kwa familia nyingi kupata huduma za msingi. "Anasema watu bado wanapata changamoto za kupata maji, umeme, na vitu vingine vya msingi kwa ajili ya matumizi ya kila siku".

Vitu vingi ambayo watu wanahitaji sana; hasa chakula na dawa za watoto kwa wale wanaosumbuliwa na maradhi. Vitu hivi ama havipatikani au inakupasa kuvitafuta katika maeneo mengine ili kuvipata.

Mapigano kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF ambayo yalianza April, 15 yaliwakosesha makaazi watu milioni 2.2 wakiwemo watoto milioni moja.

Katika ripoti iliyotolewa Alhamisi, UNICEF inasema mapigano yanayoendelea nchini Sudan yamesababisha zaidi ya watoto milioni 13 kuhitaji kwa dharura msaada wa kibinadamu.

Ripoti hiyo inasema zaidi ya watoto 330 waliuawa, na wengine 1,900 kujeruhiwa katika wiki ya kwanza ya mwezi Juni.

Forum

XS
SM
MD
LG