Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:17

Vita vya Sudan: Nchi wafadhili zakutana Geneva kujadili hali mbaya ya misaada ya kibinaadamu


Mfanyabiashara akiweka mboga zake sokoni huko Khartoum. tarehe 19 Juni 2023. Picha na AFP.
Mfanyabiashara akiweka mboga zake sokoni huko Khartoum. tarehe 19 Juni 2023. Picha na AFP.

Mkutano wa kimataifa wa wafadhili unatazamiwa kuanza mjini Geneva siku ya Jumatatu kujadili suala la Sudan, ambako mapigano yamesitishwa, lakini Umoja wa Mataifa unasema hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya baada ya miezi miwili ya vita.

Mkutano huo unaofanyika katikati ya sitisho la mapigano la siku tatu ambalo lilionekana kuleta utulivu katika mji mkuu Khartoum, baada ya kushindwa kwa mapatano ya awali ili kuhakikisha njia za ufikishaji misaada zinapatikana.

Wakazi kadhaa wa Khartoum wameliambia shirika la habari la AFP kuwa hawakusikia mashambulizi ya anga, mizinga au mapigano yoyote siku ya Jumatatu, hali ambayo ni ya nadra, wakazi hao waliochoshwa na vita wana matatizo ya uhaba wa upatikanaji wa huduma za afya, umeme, maji na mahitaji mengine muhimu.

Jeshi, linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan, tangu Aprili 15 limekuwa likipigana na Kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) (RSF) kinachoongozwa na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo, baada ya wawili hao kugombania madaraka.

Kote nchini Sudan, idadi ya vifo imeongezeka hadi kufikia 2,000, Mradi wa Armed Conflict Location and Event Data ulisema.

Mamia ya kilomita magharibi mwa Khartoum, idadi ya watu waliouwawa imefikia 1,100 huko Darfur Magharibi katika mji mkuu wa El Geneina peke yake. Kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ikililaumu "hasa" RSF.

Idadi kubwa ya watu zaidi milioni 25—ambao ni zaidi ya nusu ya wakazi wa Sudan -- wanahitaji misaada, kulingana na Umoja wa Mataifa, ambao unasema umepokea sehemu ndogo tu ya ufadhili unaohitajika sana.

Takriban watu milioni 2.5 kutoka maeneo mbalimbali nchini Sudani wamelazimika kuyakimbia maeneo yao kutokana na vita, ambavyo vimewalazimu takrikan watu 550,000 kutafuta hifadhi katika nchi jirani, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji lilisema.

Mkutano wa Jumatatu, ambao unatazamiwa kufunguliwa katika mji wa Uswizi saa tisa mchana, utazungumzia misaada inayohitajika kote Sudan na nchi jirani, ambazo kwa sasa zina mzigo mkubwa.

Umoja wa Mataifa utafanya hafla ambayo itajumuisha nchi za Misri, Saudi Arabia, Qatar, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya.

Chanzo cha habari hii nis Shirika la habaro la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG