Endapo mswaada huo utakuwa sheria, itapoteza msaada wa dola bilioni tatu kutoka Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani IFM, wizara ya fedha imesema katika waraka ambnao shirika la habari la Reuters imeuona.
Wabunge wiki iliyopita kwa kauli moja waliupitisha mswaada huo ambao uliongeza msako kwa watu wenye uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja na wale wanaotuhumiwa kuhamasisha usagaji ,ushoga au wengine wenye utambulisho wa kijinsia walio wachache.
Mswaada huo ni mojaya miswaada ya mikali sana barani Afrika, ambao sasa utapelekwa kwa rais Nana Akufo-Addo, ambaye ataamua kama ausaini kuwa sheria.
Waraka huo wa mwezi machi, umeelezea tathimini ya mjadala kati ya waziri wa fedha, gavana wa benki kuu, mkuu wa mamlaka ya kodi na maafisa wakuu, pia unajumuisha mapendekezo kwa rais.
Kupitishwa kwa mswaada huo bungeni kumekuja wakati nchi hiyo ya Afrika Magharibi ikiibuka kutoka katika mgogoro wa kiuchumi na kushindwa kulipa madeni kwa msaada wa dola bilioni tatu za mpango wa mkopo wa IMF.
Marekani ilisema “inasikitishwa sana” na pendekezo la mswaada huo na kuhimiza mapitio ya kikatiba ya mswaada huo.
Chanzo ch ahabari hii ni Shirika la habari la Reuters