Mkuu wa Shirika la IAEA aridhishwa na ziara yao Zaporizhzhia

Timu ya IAEA ilipowasili Vienna.

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki alisema Ijumaa kuwa yeye na timu yake waliweza kuona kila kitu walichotaka kukifikia katika kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia nchini Ukraine, hawakushangazwa na chochote, atatoa ripoti mapema wiki ijayo kuhusu yale aliyogundua.

“Wasiwasi wangu ni kuhusu hali ya eneo hilo – itakuwa usambazaji wa umeme na bila shaka wafanyakazi,” Rafael Mariano Grossi aliwaambia waandishi wa habari katika uwanja wa ndege mjini Vienna muda mfupi baada ya kuwasili.

Alisema ni muhimu sana kwa IAEA kuwepo kwake katika kinu hicho.

“Tunacho kifanya pale ni kuimarisha mifumo, kuangalia usalama, na ulinzi, kwa ajili ya maeneo yanayohitaji tahadhari katika kinu hicho, tukikusudia iwapo hili litakwenda vizuri, itakuwa na faida fulani, [baadhi] ya ushawishi kwa kile kitakachotokea kwa jumla

Timu ya wataalam 13 walifuatana na Grossi, amesema sita kati yao wamebaki Zaporizhzhia. Kati ya hao sita, wawili watabakia mpaka vita vitakapomalizika, ambapo amesema kutakuwa na tofauti kubwa.

“Iwapo chochote kitatokea au kutakuwa na vipingamizi vyovyote, watakuwa wanatoa taarifa – wataripoti kwetu,” Grossi alisema. “Siyo tena suala la A amesema hivi, na B amesema kile.’ Hivi sasa IAEA iko pale.”