Sehemu hiyo ni karibu na eneo lililovamiwa na Russia la kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia, ambalo hivi sasa linakaguliwa na wataalam wa nyuklia wa Umoja wa Mataifa.
Wizara hiyo pia imeeleza katika taarifa yake kuwa mazoezi ya pamoja ya kimkakati ya Russia kama vile Vostok 22 yaliyoanza Alhamisi “yamefeli kuhimili uwezo wa kijeshi kwa ngazi ya juu, katika operesheni nzito. Matukio hayo yamesajiliwa kikamilifu, hayashawishi juhudi zozote, na kimsingi yanakusidia kuwafurahisha viongozi wa Russia na watazamaji wa kimataifa.”
Timu ya UN ya wataalam wa nyuklia imemaliza ziara yake ya kwanza ya kutathmini usalama na ulinzi wa kinu cha Zaporizhzhia Alhamisi, licha ya mapigano kati ya majeshi ya Russia na Ukraine yanayoendelea karibu na mtambo huo. Wataalam wanaendelea na kazi yao siku ya Ijumaa.
Rais wa Ukraine Voldymyr Zelenskyy alisema katika hotuba yake Alhamisi usiku, “Ukraine ilifanya kila kitu kuhakikisha zoezi hili linafanyika. Lakini ni kitu kibaya kwamba wavamizi wanajaribu kuigeuza ziara hii ya IAEA – ambayo kwa kweli ni ya muhimu – kuwa ni ziara katika kinu hicho isiyozaa matunda. Ninaamini kuwa hili linaweza kuzuiliwa.”
Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Grossi, akiongoza ujumbe wa wakaguzi 14, amewaambia waandishi wa habari Alhamisi kuwa shirika hilo “linaweka uwepo wao wa kudumu” katika mtambo mkubwa zaidi wa nyuklia Ulaya. Amesema kuwa ilikuwa “dhahiri” kuwa “heshima ya eneo” la kinu cha Zaporizhzhia “imekiukwa mara kadhaa.
Grossi alisema, “Nina wasiwasi, nina wasiwasi na nitaendelea kuwa na wasiwasi kuhusu kinu hiki.”
Wakaguzi wa UN waliwasili katika kituo cha nyuklia licha ya “kuongezeka kwa harakati za kijeshi,” alisema Grossi.
Mashambulizi hayo yalilazimisha kufungwa kwa moja ya kinu cha nyuklia kabla ya kuwasili kwa wakaguzi hao, lakini Grossi alisema, “wakipima faida na hasara na kwa vile wametoka mbali, hawatasitisha uchunguzi wao.
“Tuna kazi muhimu sana ya kukamilisha,” alisema, akiongezea, “Tutaanza mara moja kufanya tathmini ya usalama wa hali ya kituo hicho cha umeme.
Baadhi ya taarifa hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.