Taifa hilo lisilo na bandari limekuwa likitawaliwa na Rais Aleksandr Lukashenko tangu 1994, ni mshirika wa karibu wa Russia. Lukashenko amekuwa akiunga mkono uvamizi wa Russia kwa Ukarine ingawa vikosi vyake havijahusika moja kwa moja kwenye mapigano hayo.
Kutokana na hilo , mataifa ya magharibi yameiwekea Belarus vikwazo ambavyo vimeathiri sekta zote za kiuchumi. Takriban wafungwa wa kisiasa pamoja na waandamanaji 1,300 waliuwawa Agosti 2020 baada ya Belarus kuanza msako mkali dhidi ya watu waliokuwa wakipinga utawala wa Lukashenko.
Hata hivyo baada ya uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine mapema mwaka huu, waandamanaji pamoja na upinzani walijitokeza barabarani kupinga wakati wakijitahidi kuwasaidia watu wa Ukraine.