Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Rafael Grossi aliwaambia waandishi wa habari "kumekuwa na ongezeko la shughuli za kijeshi, ikiwa ni pamoja na asubuhi ya leo," karibu na kiwanda hicho.
"Lakini kwa kuzingatia faida na hasara na tulipofika mpaka sasa, haturudi nyuma” Grossi aliongeza.
Ukraine na Russia zimekuwa zikishutumiana mara kwa mara kwa mashambulizi kwenye makombora katika eneo lililo karibu na kituo cha kuzalisha umeme, kituo kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya na chanzo kikuu cha nishati kwa Ukraine