Madai hayo kutoka kwa pande hizo mbili ni ya hivi karibuni katika wiki za kunyoosheana vidole kuhusiana na mashambulizi karibu na kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia, na yanakuja wakati wakaguzi kutoka Umoja wa Mataifa wakielekea eneo hilo kufanya ukaguzi wa ulinzi na usalama.
Timu ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki iliondoka Kyiv leo Jumatano huku Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Grossi akisema timu yake imepokea hakikisho kuwa itaweza kufanya kazi yao.