Mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine wa Kharkiv, umeshambuliwa kwa makombora kadhaa jumatatu asubuhi.
Gavana wa eneo hilo Oleh Syniehubov amesema kwamba jengo moja na makao makuu ya uongozi wa mji huo yameharibiwa.
Hakuna vifo vimeripotiwa.
Mkaazi wa mji huo amesema kwamba kulikuwa na mashambulizi Matano na kwamba sehemu ya nyumba yake imeharibiwa