Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:57

Wataalam wa IAEA kukagua kinu cha nyuklia cha Ukraine kilichoko hatarini


Mwakilishi wa kudumu wa Ukraine Umoja wa Mataifa (kushoto) Sergiy Kyslytsya na Balozi wa Russia UN, Vasily Nebenzya (kulia) wakihudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Usalama August 23, 2022 ulioitishwa na Russia kujadili hatari ya kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhya.
Mwakilishi wa kudumu wa Ukraine Umoja wa Mataifa (kushoto) Sergiy Kyslytsya na Balozi wa Russia UN, Vasily Nebenzya (kulia) wakihudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Usalama August 23, 2022 ulioitishwa na Russia kujadili hatari ya kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhya.

Wachunguzi wa kimataifa wamejiandaa kwa siku zijazo kufanya ukaguzi  kwenye  kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia, nchini  Ukraine  ambacho kipo hatarini wakati mapigano mapya ya mstari wa mbele yakiripotiwa Jumamosi kuzunguka eneo la mtambo huo wa nyuklia.

Timu ya wataalam kutoka Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki ya Kimataifa, au IAEA, inatarajiwa kutembelea kituo hicho cha umeme wiki hii, kulingana na mshauri wa Waziri wa Nishati wa Ukraine Lana Zerkal.

Mkuu wa IAEA, Rafael Mariano Grossi, alikaririwa akisema anataka ukaguzi ufanyikwa kwenye kinu hicho katika siku zijazo, akionya uwezekano wa kutokea janga.

FILE - Wafanyakazi wakiwa ndani ya chumba cha kuendesha mtambo wa nyuklia huko Enerhodar, Ukraine, April 9, 2013. REUTERS/Stringer (UKRAINE - Tags: ENERGY)
FILE - Wafanyakazi wakiwa ndani ya chumba cha kuendesha mtambo wa nyuklia huko Enerhodar, Ukraine, April 9, 2013. REUTERS/Stringer (UKRAINE - Tags: ENERGY)

Maafisa wana wasiwasi juu ya uwezekano wa hatari ya kuvuja miale ya nyuklia iwapo baadhi ya sehemu za mtambo huo mkubwa wa nyuklia zitashambuliwa na makombora.

Moscow ilisema inaunga mkono kazi ya IAEA lakini imekataa kuwaondoa wanajeshi wake kutoka katika mtambo huo, ili kusitisha shughuli zote za kijeshi katika eneo hilo.

Wote Russia na Ukraine zimeshutumiana kuwa zinakishambulia kwa makombora kinu kikubwa kabisa cha nyuklia barani Ulaya. Kampuni ya nishati ya serikali Energoatom ilisema Jumamosi majeshi ya Russia “yalifanya mashambulizi mara kadhaa” katika eneo hilo siku iliyopita.

Katika kukabiliana na madai hayo, wizara ya ulinzi ya Russia ilisema majeshi ya Ukraine “yalikishambulia kituo hicho mara tatu” katika siku iliyopita. “Jumla ya mabomu 17 yalipigwa,” wizara ilisema katika taarifa yake.

Kituo cha Zaporizhzhia kilitekwa na majeshi ya Russia katika siku za mwanzoni za uvamizi wa mwezi Februari na kimebakia katika mstari wa mbele wa mapambano tangu wakati huo.

Kituo hicho cha umeme kinaendeshwa na wafanyakazi wa Ukraine. Mwendesha kinu hicho pia amewashutumu wanajeshi wa Russia kwa kuwatesa wafanyakazi.

Moscow imesema inaunga mkono shughuli za IAEA lakini imekataa kuondosha majeshi yake kutoka katika kinu hicho ili kusitisha shughuli zote za kijeshi katika eneo hilo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema hali kuzunguka kinu cha Zaporizhzhia inaendelea kuwa hatarishi na si salama kabisa” baada ya kinu hicho kurejesha huduma za kusambaza umeme nchini Ukraine baada ya kukatika kwa umeme.

Kinu hicho kilisitisha usambazaji wa umeme kwa mara ya kwanza katika historia yake Alhamisi baada ya moto uliosababishwa na uharibifu wa bomu lililoathiri njia ya umeme.

Baadhi ya taarifa za habari hii zimetokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

XS
SM
MD
LG