Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:46

Zelenskiy anasema janga la mionzi limeepukika kwenye kinu cha nyuklia cha Ukraine


Picha ya kiwanda cha nyuklia cha Ukraine cha Zaporizhzhia, Agosti 22, 2022. Picha ya Reuters
Picha ya kiwanda cha nyuklia cha Ukraine cha Zaporizhzhia, Agosti 22, 2022. Picha ya Reuters

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema dunia imeepuka chupuchupu janga la mionzi Alhamisi huku mtambo wa mwisho wa kusambaza umeme kwenye kinu cha nyuklia kinachodhibitiwa na Russia cha Zaporizhzhia ukirudi kufanya kazi saa chache baada ya kukatwa.

Zelenskiy amesema mashambulizi ya makombora ya jeshi la Russia yamesababisha moto katika mashimo ya majivu karibu na kiwanda cha umeme wa makaa ya mawe ambayo yalitenganisha mtambo wa kinu hicho, kiwanda kikubwa cha nyuklia barani Ulaya, na mtambo wa umeme.

Amesema jenereta za mafuta ya dizeli zinazofanya kazi kama hakuna umeme ziliwashwa ili kuhakikisha umeme unapatikana na kuuweka mtambo huo salama.

“Kama wafanyakazi wetu kwenye kiwanda hicho hawangechukua hatua baada ya kukatika kwa umeme, basi tungelazimika kukabiliana na athari za ajali ya mionzi,” Zelenskiy amesema katika hotuba yake ya kila jioni.

Ameongeza kuwa “Russia imeweka Ukraine na wanainchi wote wa Ulaya katika hali ya hatua moja kukumbwa na janga la mionzi.”

Amesema maafisa wa shirika la kimataifa la nishati ya Atomiki (IAEA) lazima waruhusiwe kufika kwenye kiwanda hicho ndani ya siku chache, “kabla ya wavamizi kufanya kitendo kibaya ambacho hakitaziwilika.”

Russia, ambayo iliivamia Ukraine mwezi Februari, ilikiteka kiwanda hicho mwezi Machi na imekidhibiti tangu wakati huo, licha ya kuwa wafanyakazi wa Ukraine wanaendelea kukiendesha kiwanda hicho.

XS
SM
MD
LG