Mjane wa rais wa zamani wa Haiti ashtakiwa kwa mauaji

Martine Moise mke wa rais wa zamani wa haiti

Jaji mmoja wa Haiti amemshutumu mke wa rais wa zamani kwa kuhusika na mauaji ya mume wake Juvenal Moise ambaye wakati huo alikuwa rais wa nchi.

Moise alipigwa risasi na kuuwawa mwaka 2021 wakati wanaume waliokuwa na silaha walipovunja katika chumba chake cha kulala katika shambulizi lililomjeruhi mke wake, Martine.

Amri ya mahakama yenye kurasa 122 iliyotolewa kwa vyombo vya habari vya ndani ilichunguza mauaji ya Moise imewashitaki baadhi ya watu hamsini kwa kuhusika kwao katika tukio hilo.

Imemjumuisha mke wa rais wa zamani ambapo nyaraka hiyo inadai alishirikiana na waziri mkuu wa zamani Claude Joseph kumuuwa Moise ili achukue urais yeye mwenyewe.

Martine Moise ambaye bado hajajibu ombi la shirika la habari la Reuters kutoa maoni yake, ni mkoaosjai mkubwa wa utawala mpya.