Meli ya Saudia iliyozuiliwa kupakia silaha Ufaransa yawasili Italia

Meli ya Saudi Arabia Bahri-Yanbu

Meli ya Saudi Arabia iliyozuiliwa na makundi ya haki za binadamu kupakia silha katika bandari ya Le Havre nchini Ufaransa, imewasili katika bandari ya Genoa, Italia, Jumatatu.

Kundi dogo la waandamanaji limekusanyika bandarini, wakiwa wamebeba mabango yaliyo na ujumbe wa kulaani vita inayoendelea nchini Yemen.

Ijumaa (Mei 10, 2019) makundi ya kutetea haki za binadamu yalikusanyika wakishinikiza meli ya Bahri – Yanbu izuiliwe kupakia silaha katika bandari ya La Havre, ya Ufaransa.

Makundi hayo yamejitokeza kupinga usafirishaji wa silaha hizo kutokana na wasiwasi uliokuwepo hivi sasa kwamba silaha hizo zitatumika na Saudi Arabia dhidi ya raia wasio kuwa na hatia katika vita inayoendelea nchini Yemen.

Meli hiyo ya Bahri-Yanbu, ambayo imebeba shehena nyingine ya silaha iliyopakiwa Antwerp, inatarajiwa kuondoka Italia, kuelekea Jeddah, Saudi Arabia, baadaye Jumatatu.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.