Zimbabwe inawataka kuunga mkono kuondolewa marufuku ya miongo kadhaa ya biashara ya pembe za ndovu ili kukabiliana na ongezeko la idadi ya wanyama hao.
Biashara ya pembe za ndovu ilipigwa marufuku mwaka 1989 katika mkutano wa kimataifa wa biashara ya wanyama hatari baada ya idadi ya tembo kupungua kutokana na uwindaji haramu.
Lakini nchi zenye ushawishi kama vile Afrika Kusini hazitarajiwi kuunga mkono pendekezo la Zimbabwe.
Wanaamini kwamba kuna njia mbadala kudhibiti tembo bila kuruhusu uuzwaji wa pembe ikisema kuwa hiyo inahatarisha zaidi uwindaji haramu.
Baada ya mkutano katika mji wa kifahari wa Hwange, Zimbawe ilisema mapato kutokana na mamilioni ya dola ya hifadhi ya pembe itasaidia kukuza idadi ya tembo na kusaidia jumuiya zinazoishi katika eneo la hifadhi.
Wizara ya habari ya Zimbabwe imesema kwamba mwaka huu watu 60 peke yake wameuwawa na tembo ambao walitoka katika mbuga za uhifadhi wakitafuta chakula na maji.