Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 13:48

Benki kuu ya Zimbabwe yaongeza kiwango cha riba kwa asilimia 80 kudhibiti mfumuko wa bei.


Wateja wakisubiri katika foleni kuchukua pesa kwenye benki moja mjini Harare, baada ya Benki kuu ya Zimbabwe kutoa noti mpya, Novemba 12, 2019. Picha ya AP.
Wateja wakisubiri katika foleni kuchukua pesa kwenye benki moja mjini Harare, baada ya Benki kuu ya Zimbabwe kutoa noti mpya, Novemba 12, 2019. Picha ya AP.

Benki kuu ya Zimbabwe Jumatatu imetangaza kwamba imeongeza kiwango chake cha riba hadi asilimia 80 katika jitihada za kudhibiti mfumuko wa bei uliofikia kiwango cha juu sana kutokana na athari za vita vya Ukraine.

Riba hiyo imeongezeka kutoka ile ya awali ya asilimia 60 iliyotangazwa mwezi Oktoba na ni riba ya juu sana duniani, baada ya Venezuela na Argentina, kulingana na vyanzo tofauti vya takwimu.

Kulingana na mtandao wa Bloomberg unaofuatilia masuala ya kiuchumi na kifedha, riba hiyo ndiyo ya juu sana nchini humo tangu mwezi Septemba 2019 wakati benki kuu iliweka riba ya asilimia 70.

Mfumuko wa bei katika nchi hiyo yenye misukosuko ya kiuchumi ulipanda hadi asilimia 72.7 mwezi Machi kutoka asilimia 66.1 mwezi Februari.

Benki kuu ya Zimbabwe imesema ilikuta kwamba mfumuko wa bei duniani ulikuwa umeongezeka kwa sababu ya madhara ya mzozo unaoendelea kati ya Russia na Ukraine ambao umekuwa na madhara ya pili kwa bei za ndani na kimataifa.

Imesema kupanda kwa bei ya mafuta, gesi na mbolea duniani kumeathiri bila shaka gharama za ndani za uzalishaji na kuyumbisha soko la fedha za kigeni.

XS
SM
MD
LG