Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 29, 2024 Local time: 05:09

Polisi wa Zimbabwe wazuia maandamano ya upinzani


Zaidi ya wafuasi elfu moja raia wa Muungano wa upinzani nchini Zimbabwe wakizuiliwa kufanya mkutano ambapo kiongozi mkuu wa upinzani wa chama hicho Nelson Chamisa alikuwa amepangiwa kuhutubia, Machi 12, 2022 huko Marondera. (Columbus Mavh
Zaidi ya wafuasi elfu moja raia wa Muungano wa upinzani nchini Zimbabwe wakizuiliwa kufanya mkutano ambapo kiongozi mkuu wa upinzani wa chama hicho Nelson Chamisa alikuwa amepangiwa kuhutubia, Machi 12, 2022 huko Marondera. (Columbus Mavh

Polisi wa Zimbabwe mwishoni mwa wiki walikizuia chama kikuu cha upinzani nchini humo kufanya mikutano kabla ya uchaguzi wa machi 26, kujaza viti ambavyo vimeachwa wazi tangu uachaguzi mkuu wa mwaka 2018.

Polisi walipiga kambi usiku wa Ijumaa katika eneo ambako kiongozi mkuu wa upinzani wa chama cha Citizens’ Coalition for Change, Nelson Chamisa, alitakiwa kuhutubia wafuasi wake Jumamosi. Mgombea huyo mwenye umri wa miaka 44, baadae alijitokeza kutawanya umati uliokuwa ukimsubiri.

“Sisi ni chama cha Amani, chama cha utawala wa sharia. Chamisa alisema chama chake hakitaki kupigana na watu. Alisema serikali iliwanyima kibali cha kufanya mkutano, hivyo basi chama kiliomba kibali cha kuja kuelezea hilo. Aliwaambia wafuasi wake hataki siaza za Zimbabwe kusababisha kifo chochote. Kisha akaongeza kwamba jambo ambalo serikali hailifahamu ni kuwa hapa Marondera, ujio wake unatosha”.

Katika mahojiano ya Jumapili, Fadzayi Mahere, msemaji wa Citizens’ Coalition for Change, alisema chama chake hakijafurahishwa na upendeleo wa tume ya uchaguzi ya Zimbabwe, na polisi kwa kukipendelea chama tawala cha Zanu PF.

“Mkutano wetu huko Marondera ulipigwa marufuku na bado mkutano wa Zanu PF ulikuwa kwenye magari na mikutano mingine haikupigwa marufuku katika eneo hilo-hilo. Hawajawahi hata mara moja kuomba idhini au kutoa notisi kwa polisi, lakini marufuku haya ya kinyume cha sharia yanatolewa dhidi yetu. mapambano yetu ni upinzaniusio na vurugu. Hata hivyo maelfu ya watu waliojitokeza kumsikiliza rais wa chama Chamisa akizungumza inaonyesha hakuna shaka yoyote kwamba wananchi wamejiandaa kufanya chochote kinachohitajika ili kurejesha utu wao. Tunaendelea kuwasihi wafuasi wetu kujiandikisha kwa wingi kupiga kura ili tufikie lengo letu mwaka 2023 ushindi wa kishindo”.

Polisi wa Zimbabwe, siku ya Jumapili walikataa kutoa maoni kuhusu marufuku kwa chama cha Citizens’ Coalition for Change huko Marondera. Walitoa barua kwa upinzani wakisema wanahitaji muda kujiandaa ili kuhakikisha kunakuwepo Amani kwenye mkutano huo. Wiki mbili zilizopita, ghasia zilizochochewa na watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa chama tawala cha ZANU PF kwenye mkutano wa Citizens’ Coalition for Change zilisababisha vifo vya watu wawili na darzeni kujeruhiwa.

XS
SM
MD
LG