Kambi ya Kakuma iliyopo kaskazini-magharibi mwa Kenya ni mwenyeji wa zaidi ya wakimbizi 200,000 na wanaotafuta hifadhi, wakiwemo mamia ya watu wa LGBTQ ambao wanapitia "ubaguzi na manyanyaso yaliyokithiri", Amnesty na Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu kwa Mashoga na Wale wa Mapenziya Jinsia moja (NGLHRC) ilisema katika taarifa hiyo.
Wahalifu wanaweza "kutenda uhalifu wao bila ya khofu ya kuushtakiwa kabisa, hii imewezeshwa na mamlaka kwa upande kutochukua hatua", waliongeza.
Watafiti waliwahoji watu 41 kati ya mwaka 2018 na Februari 2023 ambao walielezea kukabiliwa na "uhalifu wa chuki, ghasia, pamoja na ubakaji, na ukiukaji mwingine mkubwa wa haki za binadamu".
Esther, anayejihusisha na mahusiano ya jinsia moja, mwenye umri wa miaka 41, aliwaambia watafiti kwamba alibakwa mara mbili mwaka 2018 katika kambi, mara ya kwanza na wanaume wawili waliomtishia kwa kisu, na mara ya pili na wanaume wanne waliokuwa wamefanya wizi "mbele ya mtoto wake wa kiume wa miaka saba".
Mwanamke mwingine Winnie ambaye pia anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja alisema duka lake liliharibiwa na wahalifu ambao pia walimjeruhi mmoja wa watoto wake. Alisema polisi hawakuchukua hatua ya kuridhisha kumsaidia kuwakamata waliohusika.
Matukio kama haya yalionyesha kuwa kambi hiyo, ambayo inaendeshwa na serikali ya Kenya, "bado haijawa salama kwa wakimbizi wanaotafuta hifadhi " ambao ni LGBTQ, walisema Amnesty na NGLHRC.
Chanzo cha n habari hii ni shirika la habari la AFP .