Takriban wakimbizi 60,000 wa Sudan, wengi wao wakiwa wanawake na watoto wamemiminika mpakani tangu vita vilipozuka nchini Sudan tarehe 15 Aprili, wakitafuta usalama nchini Chad, mojawapo ya nchi maskini sana duniani.
Ziara hiyo, iliyoripotiwa kwa mara ya kwanza na shirika la habari la Reuters, inaashiria kuwa hii ni safari ya kwanza kwa mkuu huyo wa USAID Samantha Power katika eneo hilo tangu mapigano yalizupo zuka kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya kijeshi lenye nguvu la Rapid Support Forces (RSF).
Power pia atakutana na maafisa wa eneo hilo wanaoratibu majibu ya mahitaji ya kibinadamu yaliyosababishwa na mgogoro nchini Sudan, Mkuu huyo wa USAID pia atakutana na jamii ya kiraia na maafisa wa serikali ya Chad, alisema msemaji huyo.
Kwa kuongeza, Power atazungumza na mashirika yanayoungwa mkono na Marekani na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na yasiyo ya kiserikali na washirika wamasuala ya kibinadamu wanaofanya kazi ya kutoa misaada kwa wakimbizi na jamii wenyeji.
Mzozo wa Sudan umesababisha vifo vya mamia ya watu na mgogoro wa masula ya kibinadamu ambao unatishia kuwayumbisha watu wengi zaidi wa kanda hiyo, pia mgogoro huo umewakosesha makazi zaidi ya watu 840,000 na kuwalazimisha takriban watu 200,000 kukimbilia nchi jirani.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters