Wanajeshi wa Sudan, chini ya mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan, walisema katika taarifa kwamba vikosi vya akiba vilifyatua risasi kwa waumini wa kikristo katika Kanisa la Mar Girgis (St George) huko Omdurman, mji pacha wa mji mkuu Khartoum.
Vikosi vya Burhan vimekuwa vikipigana tangu Aprili 15 na makamu wake wa zamani, Mohamed Hamdan Daglo, ambaye anaongoza kikosi cha wanajeshi wa akiba RSF.
Lakini pia RSF ililaumu jeshi kwa shambulio hilo, ambalo lilisababisha majeraha mabaya miongoni mwa waumini ilisema taarifa ambayo imelaani kampeni za kupotosha zinazolenga vikosi vya RSF.
Mapigano yamesumbua mawasiliano ya Sudan, na kanisala Mar Girgis halipatikana kuzungumzia suala hilo.