Israel ilishambulia ngome za wapiganaji wa kundi la Jihad Islamic katika ukanda wa Gaza kwa siku ya pili jana Jumatano na wanamgambo wa Kipalestina walirusha mamia ya roketi katika eneo la mpaka wa Israel, huku Misri ikianzisha juhudi za upatanishi kukomesha mapigano.
Wajumbe 15 wa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa walikutana Jumatano katika kikao cha faragha kuhusu ghasia za hivi karibuni.
Jumla Wapalestina 20, wakiwemo wanawake watano na watoto watano, vile vile makamanda watatu wakuu wa kundi la Islamic Jihad na washambuliaji wanne waliuawa tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi ya kabla ya alfajiri siku ya Jumanne, maafisa wa afya wa Palestina wamesema.
“Israel lazima itii wajibu wake chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu, ikiwemo kutumia nguvu sawia na kuchukua tahadhari zote zinazowezekana kuwakoa raia na mali zao katika uendeshaji wa operesheni za kijeshi, Haq alisema.