Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 15, 2024 Local time: 01:26

Rais Museveni yarudisha bungeni mswaada wa sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja


Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni Jumatano alitoa wito kwa wabunge wa nchi hiyo “kutafakari upya” sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja iliyopitishwa na bunge mwezi uliopita na kulaaniwa vikali na nchi za Magharibi.

Mswaada huo wa kupiga marufuku ushoga wa mwaka 2023 unapendekeza adhabu kali dhidi ya yeyote anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

“Ninaurudisha mswaada huo bungeni ili uungaziwe upya,” Museveni aliandika katika barua kwa bunge.

Rais Museveni aliombwa na mashirika mengi ya kimataifa na nchi kadhaa za Magharibi kutupilia mbali kile ambacho kimeshtumiwa kuwa miongoni mwa sheria kali zaidi za kupinga ushoga duniani.

Tofauti inapaswa kuwekwa katika mswaada huo “ kati ya kuwa shoga na kujihusisha na vitendo vya ushoga,” Museveni alisema katika barua yake iliyosomwa bungeni na naibu spika Thomas Tayebwa.

Imependekeza “kipengele ili kuondoa shaka, mtu anayeaminiwa au anayedaiwa au anayeshukiwa kuwa shoga ambaye hajafanya tendo la ndoa na mtu mwingine wa jinsia moja isichukuliwe kama kosa”.

Museveni aliandika “Kilicho wazi ni kwamba jamii yetu haikubali mienendo au vitendo vya ushoga.”

XS
SM
MD
LG