Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:27

Kashfa ya ngono kwenye mashamba ya chai Kenya: Makampuni yashindwa kuidhinishwa


Wafanyakazi wakichuma chai katika shamba la chai nje ya Kericho, Februari 6, 2008. Picha na shirika la habari la REUTERS/Peter Andrews.
Wafanyakazi wakichuma chai katika shamba la chai nje ya Kericho, Februari 6, 2008. Picha na shirika la habari la REUTERS/Peter Andrews.

Shirika la kimataifa limesema kuwa limesitisha uidhinishaji wa kampuni mbili kubwa za chai duniani kufuatia uchunguzi wa kashfa ya manyanyaso ya kingono nchini Kenya.

Muungano wa Rainforest Alliance ulitangaza hatua hiyo siku ya Alhamisi dhidi ya makampuni ya James Finlay(Kenya) Ltd na ekaterra Tea Kenya Plc, ikimaanisha kuwa chai inayouzwa na makampuni hayo hayawezi tena kutumia cheti cha shirika hilo lisilo la kiserikali.

Muungano huo – ni moja ya mashirika makuu ya uidhinishaji wa bidhaa za maendeleo endelevu -- ulisema ulianzisha uchunguzi baada ya makala ya BBC iliyotangazwa mwezi Februari iliyoangazia madai ya kuenea kwa manyanyaso ya kingono kwenye mashamba ya chai nchini Kenya uliyoyahusisha moja ya makampuni makubwa ya uuzaji wa chai duniani.

Zaidi ya wanawake 70 waliiambi BBC kuwa kwa miaka mingi walikuwa wakinyanyaswa kingono na wasimamizi wao.

BBC ilisema ilizungumza na dazeni ya waathirika ambao walisema hawakuwa na la kufanya bali kukubali matakwa ya ngono kutoka kwa wasimamizi wao au kupoteza ajira.

Mmoja wa waathirika aliripotiwa kuambukizwa UKIMWI na msimamizi wake, wakati wengine walipata ujauzito.

Aidha msimamizi mmoja alishtakiwa kwa kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikuwa akiishi kwenye eneo moja katika mashamba hayo.

"Kwenye mashamba yote mawili ya chai, ukaguzi ulithibitisha kuwepo kwa ukiukwaji wa vigezo vya kijamii na usimamizi wa Kiwango cha Kilimo Endelevu cha Msitu wa Mvua," muungano huo ulisema katika taarifa yake ya kutangaza kusitisha uidhinishaji wake kwa kampuni hizo mbili.

Uamuzi huo -- ambao ulianza kutumika awali katika kipindi cha miezi mitatu -- unamaanisha kuwa makampuni hayo hayawezi kuuza au kusafirisha bidhaa kwa kutumia cheti Kilicho idhinishwa na Rainforest Alliance.

Waendesha mashtaka na wabunge nchini Kenya walisema mwezi Februari kuwa wangechunguza tuhuma hizo, lakini hakuna hatua za mahakama zilizochukuliwa.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG