“Hii ni leseni ya kwanza ya kutuma na kupokea pesa kwa simu ya mkononi inayopewa mwekezaji wa kigeni nchini Ethiopia, Benki ya taifa ya Ethiopia ilisema katika taarifa.
Kampuni ya mawasiliano ya Ethiopia, Ethio Telecom, tayari inatoa huduma ya kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu ya mkononi iitwayo Telebirr, iliyopewa jina la sarafu ya taifa, birr.
Safaricom ilianzisha kwa mara ya kwanza hudumu yake ya kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu ya mkononi ijulikanayo kama M-Pesa nchini Kenya mwaka wa 2007 na imekuwa njia muhimu kwa kulipa ada na kutuma pesa.
Mfumo huo unatumiwa hivi sasa na watu milioni 51 katika nchi saba za Afrika, kulingana na Safaricom, ambayo inakadiria kuwa M-Pesa inachangia kwa asilimia 40 ya mapato yake.