Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:14
VOA Direct Packages

Museveni aamuru mswaada wa LGBTQ ufanyiwe marekebisho kabla ya kuutia saini kuwa sheria


Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekataa kutia saini mswaada wenye utata  dhidi ya mashoga, ambao umezungumzia adhabu ya kifo katika baadhi ya kesi, na kutaka kuwa ni vyema ufanyiwe marekebisho.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, uamuzi wa Museveni ulitangazwa Alhamisi jioni baada ya kikao cha wabunge wa chama chake tawala, ambao karibu wote waliunga mkono kuidhinishwa na wabunge mwezi uliopita.

Taarifa zimeongeza kusema kwamba wabunge hao wamekubaliana kuurejesha bungeni ili ufanyiwe marekebisho. Kwa mujibu wa video iliyorushwa na televisheni ya taifa ya UBC, Museveni anaonekana akipinga ushoga akiwa mji mkuu Kampala, akisema kwamba, “ Ulaya imepotea.

Wanataka sisi tupotee pia.” Museveni pia aliwasifu wabunge kwa kupitisha mswaada huo, ambao umezua ukosoaji mkubwa wa kimataifa.

XS
SM
MD
LG