Marekani na Afrika kuangalia njia bora ya kupunguza pengo la uaminifu kati yao

Mkutano wa viongozi wa Afrika, Washington, DC.

Rais Joe Biden atakuwa mwenyeji wa dazeni ya viongozi wa Afrika hapa Washington wiki hii wakati White House ikiangalia kupunguza pengo la uaminifu na Afrika –ambalo limekuwa kubwa baada ya miaka kadhaa ya mashaka kuhusu nia ya Marekani kwa bara hilo. Khadija Riyami anaripoti zaidi.

Mkutano huu utakuwa ni mkusanyiko mkubwa sana wa kimataifa hapa Washington tangu kuanza kwa janga la Covid-19. Maafisa wanawaonya wakazi kuheshimu vizuizi vya barabarani na kuimarishwa kwa uinzi wakati wakuu na viongozi wa nchi 49 pamoja na Biden wakiwa wanazunguka mjini.

Mazungumzo yalitarajiwa kulenga kuhusu virusi vya corona, mabadiliko ya hali ya hewa, matokeo ya uvamizi wa Russia nchini Ukraine kwa Afrika, biashara namengi zaidi. Mkutano wa biashara kati ya Marekani na Afrika, kutafanyyika mikutano ya viongozi katika vikundi vidogo vidogo, mwenyeji atawakaribisha kwa chakula cha viongozi wa Afrika huko White House na pia kushiriki katika vikao vingine na viongozi wakati wa mkutano huo.

Msemaji wa White House, Karine Jean-Pierre

Karine Jean-Pierre, Msemaji wa White House anaeleza:“Jumatano, rais anatazamia kuwa mwenyeji katika mkutano wa viongozi wa Afrika na Marekani. Mkutano huu utasisitiza jinsi Marekani inavyoangalia thamini zetu kwa ushirikiano na Afrika ni suala ambalo ni changamoto ya ulimwengu na fursa, pamoja changamoto za ulimwengu na fursa, pamoja na nia ya dhati ya utawala wa Biden katika kufufua tena ushirika wa ulimwengu na ushirikiano.”

Biden ametumia muda mwingi katika miaka yake miwili ya kwanza madarakani kwa kujaribu kuwatoa wasi wasi kwa wale ambao wako katika uwanja wa kiamtaifa kuhusu uongozi wa Marekani miaka minne baada ya sera ya mambo ya Donald Trump ya “America Kwanza.” Huku mkutano wa viongozi – ni kufuatilia mkutano kama huu uliofanyika miaka minane iliyopita uliofanywa na Rais Barack Obama – Biden alikuwa na fursa na kuondoa wasi wasi huko Afrika kuhusu iwapo Marekani ina nia ya dhari kuhusu kuimarisha uhusiano.

Juhudi za Biden kuyaleta karibu mataifa ya Afrika kwa Marekani katika wakati huu wenye mambo mengi, huku utawala wake umeeleza bayana kwamba unaamini kwamba harakati za China na Russia barani Afrika ni jambo la kutia wasi wasi sana kwa maslahi na Marekani na Afrika..

Katika mkakati wake wa barani Afrika chini ya jangwa la Sahara uliozinduliwa mwezi Agosti, utawala wa Biden ulionya kwamba China, ambayo imetumbukiza mabilioni katika nishatia, miundo mbinu na miradi mingine barani Afrika, inaliona eneo hilo kama uwanja wa Beijing ambao wanaweza “kubadili kanuni na utaratibu wa kimataifa, kusukuma maslahi yao madogo ya kibiasharan na kisiasa, kudumaza uwazi.”

Rais wa Russia Vladimir Putin

Utawala pia unadai kwamba Russia, ni muuzaji maarufu wa silaha barani Afrika, inaliona bara hilo kama ni mazingira muafaka kwa Kremlin makampuni ya taifa na binafsi ya kijeshi ili kulenga katika kuleta ukosefu wa utulivu kwa mikakati yao wenyewe na manufaa ya kifedha.

Bado, maafisa wa utawala wanasisitiza kwamba wasi wasi kuhusu China na Russia hayatatawala mazungumzo.

Rais alitarajiwa kushiriki katika vikao na viongozi katika kuhamasisha usalama wa chakula na mifumo stahimiliv ya chakua. Afrika imeathiriwa sana na kupanda kwa bei za vyakula ulimwengun ambazo zimesababishwa kwa kiasi na kushuka kwa shehena ya nafaka ambayo Ukraine ni muuzaji mkubwa sana.

Nchi nne ambazo zimesimamishwa kutoka Umoja wa Afrika, Guinea, Sudan, Mali na Burkina Faso – hazijakaribishwa katika mkutano kwa sababu ya mapinduzi katika mataifa hayo yaliyopelekea mabadiliko ya uongozi kinyume cha katiba. White House pia haijaikaribisha Eritrea taifala Afrika Mashariki. Washington haina uhusiano kamili wa kidiplomasia na nchi hiyo.