Mwaka huu pekee bara la Afrika limeshuhudia mafuriko mabaya sana huko Afrika Kusini na miaka kadhaa ya ukame mbaya huko Pembe ya Afrika.
Mataifa ya Afrika katika mkutano wa COP27 yamesukuma sana kwa mataifa tajiri kulipa fidia ya hali ya hew ana kuchangia katika mfuko wa “hasara na uharibifu” .
Katika taarifa ya pamoja, China, Brazil, India na Afrika Kusini zimezishutumu nchi tajiri kwa viwango visivyo vya kawaida vya matumizi ya mafuta yatokanayo na mizoga na mimea wakati wakizisukuma nchi zinazoendelea kuwa za kijani.
“Ukweli halisi ni kwamba hakuna nchi hata moja tajiri imefanikiwa ‘kuendeleza’ hatua ya kujizuia kwa njia yoyote katika matumizi ya kaboni, bado nchi zote zinazoendelea hivi sasa zinahitaji njia mpya ya kufanikisha kipato cha juu chini ya lengo la digrii 1.5.” Wei Shen, mtalaamu wa hali ya hewa katika Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo Uingereza ameiambia VOA.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni alibandika katika mtandao wa kijamii akiishutumu EU kwa “viwango vya Magharibi visivyo na uwiano,” akielezewa kwamba nchi za Ulaya zinarejea kwenye uchimbaji makaa.
Tangu vita vya Ukraine na bila ya gesi ya Russia, Ujerumani imekuwa ikitegemea zaidi maklaa kwa nishati ili kuweza kukabiliana na kipindi cha baridi kali sana.
Serikali nyingi za kiafrika zinakubaliana na ukweli kwamba wakati bara hilo linahusika na kiasi cha 3% ya hewa chafu ulimwenguni pia wanaambiwa kuachana na matumizi ya nishati “fossil Fuels” ambayo baadhi wanasema inahitajika sana kwa maendeleo ya eneo hilo ambako watu wachache chini ya nusu wana fursa ya umeme.
Migawanyiko juu ya fidia
Marekani imeisukuma China – ambayo hivi sasa ni mtoaji mkubwa sana wa gesi chafu duniani na mteja wa makaa ya mawe – kujumuishwa katika kundi la mataifa yanayohusika katika utoaji wa fidia. Ikiwa ni nchi ya pili yenye uchumi kubwa duniani, China ni vyema illipe mgao wake, Washington inasema.
Lakini wakati China inasema inaunga mkono nchi zinazoendelea katika azma yako ya kutaka ufadhili, haitachangia fedha kwasababu – kwa mujibu wa viwango vya Benki ya Dunia – ni nchi inayoendelea pia.
“Katika mkutano wa COP27, according to World Bank criteria — it's a developing country too.Balozi wa China kuhusu hali ya hewa Xie alisema kwamba China haina jukumu lolote la kutoa. Ufadhili wa L & D, lakini nchi yake iko tayari kuziunga mkono nchi za kipato cha chini kwa ajili ya L & D ambayo imesababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa,” Leo Alice Bian, mhadhiri katika chuo cha Uchumi Londo ameiambia VOA.
“Jaribio la Marekani kwa msimamo wake kwa China kama nchi ilioendelea kwa kweli halitakuwa na nguvu huko Afrika kwasababu upande wa Afrika unakubali…… kwamba China ni vyema itendewe kama nchi inayoendelea,” alisema Paul Nantulya, mchambuzi katika African Center for Strategic Studies huko Washington.
Hiyo ni kwasababu Magharibi inahusika na uzalishaji wa “kihistoria na mkusanyiko” wa hewa chafu kutoka katika mapinduzi ya viwanda ambayo yalisababisha hali ya joto joto ulimwenguni ambayo dunia inaishuhudia hivi leo, alisema.
Wakati nchi nyingi zinazoendelea zinailaumu Magharibi kwa mabadiliko ya hali ya hewa, hata zikisema China pia ni muathirika, Ovigwe Egeugu, mchambuzi katika kituo cha ushauri cha Development Reimagined chenye makao yake mjini Beijing ameiambia VOA: “Imekubalika na wengi – hata Beijing – ambapo China kupanda kwake kuwa chini ya pili yenye uchumi mkubwa sana duniani umekuja kwa gharama ya mazingira.”
"China yenyewe iko katika kitendawili,” Nantulya alisema.
“Ni mchangiaji mkubwa duniani wa hewa chafu……. Hat ahivyo pia. Imeibuka kuwa muwekezaji mkubwa sana katika nishati safi dunani.”
Barabara ya Kijani
Rais wa China Xi Jinping aliapa katika Umoja wa Mataifa mwaka jana kwamba nchi yake kamwe haitafadhili tena nishati ya maka nje ya nchi, huku ikilenga badala yake kweye nishati safi, ingawaje njia ya kufikia nishati ya kijani ina baadhi ya vikwazo.
Eneo lamaalum la kiuchumi huko Musina, Afrika Kusini ambalo linaungwa mkono na China, awali lilijumuisha kituo cha umeme unaotumia makaa ya mawe.
“Mipango ya awali kujenga kituo cha umeme cha makaa yam awe ilisimamishwa. Kituo cha nishati ya umeme wa jua ambacho kitatoa Megawati 1000 kilipangwa kuongezea mahitaji mchanganyiko ya nishati…. Kwa muwekezaji wa China,” Shavana Mushwana, msemaji wa eneo hilo ameiambia VOA kwa njia ya barua pepe.
Hata hivyo, Patrick Bond, mtaalamu wa siasa ya uchumi katika chuo kikuu cha Johannesburg, alisema hata bila ya kiwanda kipya cha umeme unaotumia makaa, bado maendeleo hayo yatachangia katika kuwa mchafuzi wa hewa, akielezea “kuna mahitaji makubwa sana huko…...kwa vile umeme wa ziada unahitajika kuendesha viwanda vikubwa sana na uchafuzi huo hautoki kutoka katika baadhi ya vituo vidogo vinavyotumia sala,” kwahiyo Special Economic Zone litahitaji kutumia kwa kiasi kikubwa gridi ya umeme ya Afrika Kusini.
Ushahidi wa China katika “Green Silk Road” unaweza kuonekana kote barani humo. Katika nchi ambayo inahitaji sana nishati Afrika Kusini, kampuni ya kichina imeanzishwa De Aar huko Northern Cape. Nchini Kenya, China inafadhili kiwanda cha umeme cha megawati 15 ambacho kitatumia umeme wa jua huko Garissa, na huko Jamhuri ya Afrika ya Kati , kiwango cha umeme wa jua kimekamilika mwaka huu na kinatoa kiasi cha 30% ya mahitaji ya umeme katika mji mkuu.
“Mwezi Septemba mwaka 2021, rais wa China alitangaza katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba China itasimamisha uwekezaji katika makaa, kwenye miradi ya nje ya nchi, na watalenga uwekezaji zaidi katika nishati safi,” Tony Tiyou mkuu wa Renewables huko Afrika ameiambia VOA. “Kwa hakika wamelitekelza hilo.”
Miradi 15 ya makaa iliyokuwa inafadhailiwa na China tangu wakati huo imefutwa, ingawaje mingine tayari iliyokuwa katika hatua za ujenzi inaendelea, Nantulya alisema.
Aliongezea kwamba mabenki ya China, “haraka yalijibu kuhusu mabadiliko katika sera. Benki ya Exim, kwa mfano, ilitoa dola milioni 425 kwa bondi za kijani ambazo zilitengwa kwa ajili ya uwekezaji wa nishati safi.”
China iliwekeza dola bilioni 380 katika nishati safi mwaka 2021, zaidi kuliko nchi yoyote nyingine, na inahusisha karibu nusu ya uwekezaji kwa nishati mbadala.
“China ina nia ya dhati katika kujihusisha na soko la nishati mbadala barani Afrika” alisema Wei.
Tuhuma za unafiki
Wachambuzi walielezea lengo la Beijing kwa nishati ya kijani linakuja baada ya kesi kadhaa za awali za miradi mbali mbali huko Afrika ambapo wana mazingira waliyashutumu makampuni ya China kwa kucahfua mazingira na kuharibu makaziya wanyama pori kwa operesheni zao za uchimbaji madini na miradi ya miundo mbinu.
Hivi sasa, china imenahusika na mradi mkubwa wa mafuta ghafi huko Uganda, Tanzania na kampuni ya Ufaransa. Licha ya upinzani kutoka Umoja wa Ulaya ambao ina wasi wasi kubwa bomba hilo la mafuta litaharibi hali ya hew ana mazingira.
Rais Museveni wa Uganda aliishambulia EU kwa kujaribu kuingilia kati. Museveni ni miongoni mwa idadi kubwa ya wanasiasa wa kiafrika ambao mara kwa mara wanaiona Magharibi kama inawafndisha na ina undumila kuwili kwenye mabadiliko ya hali ya hewa, wakidai kuwa matumizi ya nishati ya ‘fossil fuels’ ndyo imeifanya Magharibi kutajirika na kusababisha mzozo wa hali ya hewa.
Nchi tajiri hata hivyo, zimegawanyika kuhusu suala la fidia.