Tathmini ya awali ya kamandi hiyo ni kuwa shambulizi hilo limemuua kiongozi wa al-Shabaab na hakuna raia aliyeuawa au kujeruhiwa.
Kamandi ya Marekani Afrika inachukua tahadhari kubwa kuepusha vifo vya raia. Kuwalinda raia wasio na hatia ambao ni sehemu muhimu ya operesheni za kikosi hiki kuhakikisha usalama zaidi na utulivu Afrika.
Al-Shabaab ni mtandao mkubwa kabisa na wenye harakati zaidi za al-Qaeda duniani na imethibitisha nia yake na uwezo wake wa kuyashambulia majeshi ya Marekani na inatishia maslahi ya usalama wa Markeani.
Kamandi ya Marekani Afrika,kikiwa na washirika wake, inaendelea kuchukua hatua kuzuia kikundi hiki cha kigaidi kiovu kupanga na kutekeleza mashambulizi kwa raia.
Somalia itaendelea kuwa ni kituo muhimu kwa mazingira salama ya Afrika Mashariki. Majeshi ya Kamandi ya Marekani Afrika yataendelea kufundisha, kushauri na kutoa vifaa kwa majeshi ya washirika kuwapa nyenzo za kuidhoofisha al-Shabaab.
Kamandi ya Marekani Afrika itaendelea kutathmini matokeo ya operesheni hii na itatoa taarifa ya ziada kama itkavyohitajika. Maelezo kamili kuhusu pande zilizohusika na vifaa vilivyotumika havitatajwa kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa operesheni zake.
Kamandi ya Marekani Afrika, yenye makao yake makuu Stuttgart, Ujerumani, na washirika wake, inapambana na watenda uovu na vitisho vya kimataifa, inakabiliana na majanga, na kuimarisha majeshi ya usalama kwa ajili ya kusukuma mbele maslahi ya taifa la Marekani na kuhamasisha usalama wa kanda, utulivu na mafanikio.