Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:09

Somaliland yaahirisha uchaguzi wake wa urais  hadi mwaka ujao


Wanawake huko Hargeisa Somaliland wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura.
Wanawake huko Hargeisa Somaliland wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura.

Tume ya uchaguzi ya jimbo lililojitenga la Somalia, la Somaliland imetangaza leo Jumamosi kwamba itaahirisha uchaguzi wake wa urais  hadi mwaka ujao, badala ya kuufanya mwezi Novemba wakati muhula wa rais aliyeko madarakani utakapomalizika.

Mwezi Agosti maandamano yaliosababisha mauaji yalizuka katika jimbo hilo ambapo waandamanaji walitaka uchaguzi ufanyike mwezi Novemba wakati kukiwa na dhana kwamba Rais Muse Bihi Abdi alitaka kuchelewesha uchaguzi ili kuongeza muda wa mhula wake.

Uchaguzi sasa utafanyika katika baada ya miezi tisa kuanzia Oktoba hadi Julai ijayo kwa sababu tarehe iliyopangwa ya sasa ya Novemba 13 haiwezi kufanyika kutokana na muda, matatizo ya kiufundi na kifedha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Somaliland (SLNEC) iliandika kwenye Twitter Jumamosi.

Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka 1991 lakini uhuru wake haujapata kutambuliwa kimataifa. Jimbo hilo limekuwa na amani zaidi kuliko majimbo mengine ya Somalia ambayo kwa miongo mitatu inakumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Katika ghasia za mwezi Agosti kati ya maafisa wa usalama na waandamanaji wa upinzani takriban watu watano waliuawa na 100 kujeruhiwa.

Katika mkutano na waandishi wa habari baada ya tangazo la SLNEC, Wadani, moja kati ya vyama vya upinzani kilichongoza maandamano hayo ya Agosti, kimeeleza kuridhika kutokana na tarehe hiyo mpya.

XS
SM
MD
LG