Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:21

Mwanajeshi mmoja auawa na sita wajeruhiwa katika shambulio la bomu Somalia


Mlipuko kwenye gari Somalia.Mei 11, 2022 (AP Farah Abdi Warsameh)
Mlipuko kwenye gari Somalia.Mei 11, 2022 (AP Farah Abdi Warsameh)

Mwanajeshi mmoja aliuawa na takriban wengine sita kujeruhiwa nchini Somalia siku ya Jumapili wakati mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua katika kambi ya kijeshi magharibi mwa mji mkuu Mogadishu, mwanajeshi na mfanyakazi wa hospitali waliambia Reuters.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alivaa sare za kieshi na kujiunga na wenzake wengine walipokuwa wakiingia kwenye kambi ya kijeshi mapema Jumapili kabla ya kulipua vilipuzi, Kapteni Aden Omar, mwanajeshi katika kituo hicho aliambia Reuters.

Aliongeza kusema kwamba “Tulipoteza askari mmoja na wengine kadhaa kujeruhiwa. Mlipuaji alijilipua kwenye kituo cha ukaguzi."

Muuguzi mmoja katika Hospitali ya Madina mjini Mogadishu amesema kuwa wamepokea mwanajeshi mmoja aliyefariki na wengine sita ambao walijeruhiwa.

Haijabainika mara moja ni nani aliyetekeleza shambulio hilo lakini kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al Shabaab mara kwa mara hutekeleza mashambulizi ya mabomu na bunduki nchini Somalia na kwingineko.

XS
SM
MD
LG