Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:45

Mabomu mawili ya kwenye gari yateguliwa Somalia


Gari lililoharibiwa na bomu Somalia kwenye picha ya maktaba
Gari lililoharibiwa na bomu Somalia kwenye picha ya maktaba

Wakazi wa mji wa Beledweyne ulioko takriban kilomita 337 kaskazini mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, wamemwambia mwanahabari wa VOA kwamba mabomu mawili ya kwenye gari yameteguliwa Jumatatu.

Hilo limetokea kwenye makao makuu ya utawala wa kieneo wa Lamagalay, ambako gavana pamoja na maafisa wengine wa serikali wanafanyia kazi zao. Hata hivyo hakuna ripoti za kina zilizotolewa kuhusiana na maafa au majeruhi kufuatia shambulizi hilo.

Tukio hilo limetokea saa chache baada ya sarikali ya Somalia Jumapili jioni, kutangaza kwamba kiongozi wa ngazi ya juu wa al Shabab aliuwawa katika operesheni kwenye eneo la Haramka katikati mwa Jubaa hapo Octoba mosi.

Kupitia taarifa , wizara ya habari ilisema kwamba Abdullahi Nadir ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa al Shabab aliuwawa wakati wa operesheni ya jeshi la serikali likishirikiana na vikosi vya kimataifa. Wakazi wa mji huo katika siku za karibuni wamekuwa kwenye mstari wa mbele katika kupambana na wanamgambo wa al Shabab.

XS
SM
MD
LG