Mjumbe wa masuala ya hali ya hewa wa Marekani John Kerry ameonya dhidi ya kuwekeza katika miradi ya muda mrefu ya gesi barani Afrika huku nchi za eneo hilo baadhi zikitarajia kuibua ugunduzi wa hivi karibuni wa mafuta ya gesi zikipambana na jinsi ya kuimarisha maendeleo yao ya nishati safi. “ hatusema kwamba kahuna gesi”, Kerry ameliambia shirika la habari la Reuters pembeni ya mkutano wa mawaziri wa Afrika wa mazingira katika mji wa Dakar , Senegal siku ya Alhamisi. “ Tunachosema ni kwamba katika miaka michache ijayo gesi inachukua nafasi ya makaa ya mawe au kuchukua nafasi ya mafuta , alisema hayo waziri wa zamani wa mambo ya nje na mgombea wa urais kupitia chama cha Democrat akiongeza kuwa gesi inaweza kutumika kama mpito kwa vyanzo safi vya nishati. Lakini Kerry amesema baada ya mwaka 2030 itakuwa muhimu kukamata uzalishaji wa gesi pia. Ufadhili wa mafuta na gesi katika bara la Afrika imekuwa swala muhimu kwa nchi ambalo wanapanga kusukuma wakati wa Mkutano wa hali ya hewa utakaofanyika Misri mwezi Novemba . Senegal na nchi nyingine katika eneo zina mpango wa kuzalisha mafuta na gesi ambapo wanatarajia zitasaidia kuinua uzalishaji wa mafuta , viwanda vinavyotumia umeme , na kutokomeza umasikini wa nishati.