Magoli ya Uholanzi yalifungwa na Cody Gakpo and Davy Klaassen. Mchezaji nambari 8 alifanya vyema kupata krosi ya nyota wa Barcelona Frenkie de Jong mbele ya kipa wa Senegal, Edouard Mendy, na kuukwamisha mpira wavuni. Hadi mwisho wa mchezo Uholanzi 2 Senegal 0.
Mabingwa hao wa Afrika walijikuta katika wakati mgumu na kuthibitisha kwamba pengo la mkali wao Sadio Mane bado halijazibika na itakuwa vigumu kufanya hivyo.
Siku ya Ijumaa Senegal itacheza na Qatar wakati Uholanzi itamenyana na Ecuador. Hiyo ndio itakuwa nafasi ya Simba hao wa Teranga kulipiza kisasi.
Na wakati huo huo timu ya Uingereza waliweka historia kwa kuichabanga Iran jumla ya mabao 6-2. Katika mchezo huo mchezaji Bukayo Saka alipachika mabao mawili huku Jude Bellingham, Raheem Sterling, Marcus Rashford na Jack Grealish wakiongeza mabao mengine . Kocha wa timu hiyo Gareth Southgate alikasirishwa na timu yake kumruhusu Mehdi Taremi wa Iran kuifungia timu yake mabao mawili
Wakati huo timu ya taifa ya Marekani imetoka sare na Wales kwa jumla ya bao 1-1. Marekani bao la kuongoza kupitia kwa Timothy Weah mtoto wa Rais wa Liberia na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa nchi hiyo George Weah kunako dakika ya 36.
Marekani timu yenye wachezaji wengi vijana ikiwa na nahodha kinda wa miaka 23 imeonyesha moyo wa kupambana dhidi ya Wales. . Timu hii ya Marekani ni ya pili kwa vijana wadogo baada ya Ghana.
Hatimaye Wales walifanikiwa kusawazisha kunako dakika ya 82 kwa mkwaju wa penati kupitia mkongwe Gareth Bale.
Marekani walidhibiti mchezo huo kwa asilimia 87 wakati Wales walimiliki kwa asilimia 76.