Utawala wa Biden umepuuza ushawishi wa China na Russia ambao unaendelea kuongezeka barani Afrika lenye takribani zaidi ya watu bilioni 1.3.
Maafisa wa White House badala yake wanazingatia sana namna ya kuboresha ushirikiano wa Marekani na viongozi wa Afrika.
Msemaji wa White House Kaine Jean Pierre, amesema kwamba kongamano la wiki hii ni fursa nzuri ya kuimarisha ushirikiano na bara la Afrika hasa katika biashara, Afya na usalama.
Biden anatarajiwa kutumia fursa ya kongamano hilo la viongozi wa Afrika, kutangaza wanachama wa kudumu wa Afrika katika kundi la nchi 20 zenye nguvu kubwa duniani.
Juhudi za Biden kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na mataifa ya Afrika zinajiri wakati ambapo utawala wake umesema kwamba unaamini kuwa ushawishi wa China na Russia barani Afrika unastahili kuzingatia sana maslahi ya Marekani na Afrika.