Marekani: Dunia yasubiri kwa shauku matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhula

Rais wa Marekani Joe Biden (kulia) na Rais wa zamani Donald Trump

Mustakbali wa programu za utawala wa Biden na juhudi nyingine zinategemea kwa kiasi  kikubwa na matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa Novemba 8 ambapo viti vyote katika Baraza la Wawakilishi na viti 35 vya Baraza la Seneti vinapigiwa kura..

Kwa wingi walio nao sasa Wademokrat katika Baraza la Wawakilishi wakiwa na viti tisa zaidi, na Baraza la Seneti linadhibitiwa na chama hicho ikishikiliwa na Makamu wa Rais Kamala Harris mwenye kura ya “maamuzi” inapohitajika, udhibiti wa Capitol Hill una nafasi yake katika siku hii ya uchaguzi.

Wachambuzi wanaangazia kinyang’anyiro cha nafasi sita katika Baraza la Seneti ambapo kura za maoni zinaonyesha “hakutabiriki” - hali ambayo wapiga kura wasiokuwa na maamuzi na wanaobadilisha maamuzi wataamua nani atakaye shikilia Washington.

Ushindani mmoja mkuu uko Georgia, ambako Seneta Mdemokrat aliyeko madarakani Raphael Warnock anapambana na mgombea mpya bingwa wa mpira wa miguu Hershel Walker. Warnock alichukua nafasi hiyo 2020 katika duru ya pili ya uchaguzi.

Seneta mwingine machachari yuko Nevada. Kura za maoni za Republikan zinamweka mgombea wake, Adam Laxalt akiongoza kwa pointi chache, lakini kura nyingine za maoni zinaonyesha mgombea aliyoko madarakani Seneta Gatherine Cortez Masto akiongoza.

Seneta wa Wisconsin Mrepublikan anayetetea kiti chake Ron Johnson alikuwa akiongoza katika kura za maoni za awali, lakini kura za hivi karibuni zinaonyesha ushindani na Mdemokrat Mandela Barnes ni wa karibu sana.

Katika jimbo dogo la kaskazini mashariki la New Hampshire, Mdemokrat anayetetea kiti chake Seneta Maggie Hassan anaongoza juu kidogo dhidi ya mpinzani wake Mrepublikan Don Bolduc.

Pennsylvania - ambalo ni jimbo lililoasisi demokrasia na kujipatia jina la “Keystone State” limeshuhudia vyama vyote viwili vikipambana kukamata “viti vilivyowazi” kimoja ni cha seneta aliyestaafu, Mrepublikan Pat Toomey. Chama cha Republikan kimemtuma daktari aliye na kipindi cha televisheni na mwenye uraia pacha wa Marekani na Uturuki Mehmet OZ, ambaye kura za maoni zimeenda vizuri licha ya upinzani mkubwa kutoka kwa hasimu wake, Luteni Gavana wa Pennsylvania John Fetterman, ambaye alipata kiharusi mwezi Juni lakini aliendelea kugombea nafasi hiyo.

Mgombea anayetetea kiti chake Arizona Mdemokrat Seneta Mark Kelly, Rubani wa zamani wa safari za anga za mbali, anapambana na Mrepublikan Blake Masters. Watabiri wanampa ushindi Kelley ushindi katika jimbo ambalo ugavana unaweza kuwa ni ushindi kwa Mrepublikan Kari Lake, ambaye amemkubali Donald Trump na madai ya rais huyo wa zamani kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais ya 2020 haya kuwa ya kweli.

Kwa sababu Baraza la Seneti hivi sasa lina Warepublikan 50 dhidi ya Wademokrat 48 na wagombea huru wawili ambao wanapiga kura upande wa Wademokrat, kiti kimoja wakikipata Warepublikan kinamuondolea kura ya maamuzi Harris na wanachukua baraza hilo.

Katika Baraza la Wawakilishi, chama cha Demokratik hivi sasa kina viti 222 wakati Warepublikan wanadhibiti viti 214. Kwa hiyo, ili Warepublikan kuchukua udhibiti wanahitaji viti vitano, na ndiyo, “nguvu ya fedha” ya serikali kwani matumizi yote ya serikali kuu yanatoka katika baraza la wawakishi.

Kwa sababu hiyo, ushindi wa Republikan katika Baraza la Wawakilishi utakiwezesha chama cha upinzani kuzuia matumizi ya uongozi wa Biden kwa programu zilizokuwa zimepitishwa na kuungwa mkono na Wademokrats.