Badala yake mahakama kuu imerudisha shauri hilo kwa mahakama ya chini kusikilizwa zaidi.
Lakini uamuzi huo wa mahakama kuu pia umekuwa pigo kwa upande mwingine kwa kuonyesha kwamba rais hana kinga ya moja kwa moja inayomwezesha kukataa kutoa rekodi zake za fedha.
Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani na Waendesha mashitaka wa jimbo la New York ambako rais Trump amekuwa akiishi na kuendesha biashara zake kwa miaka mingi waliwasilisha madai ya kumlazimisha Trump atoe rekodi zake za ulipaji kodi kwa Bunge na mahakama ya New York.
Uamuzi wa mahakama kuu leo ina maana waendesha mashitaka wa New York hawajafanikiwa kupata rekodi hizo kwa sasa lakini wana nafasi nyingine ya kuwasilishamadai yao katika mahakama ya chini.
Waendesha mashtaka wa New York wanataka pia kupata rekodi za fedha za rais Trump ambazo zinashikiliwa na kampuni yake ya uhasibu na benki.