Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:03

Idadi ya waliouawa Ethiopia yafikia 166 - Polisi


Moshi waonekana kwa mbali mjini Addis Ababa, Ethiopia, wakati wa ghasia na maandamano kufuatia kuuawa kwa mwanamuziki maarufu Haacaaluu Hundeessaa.
Moshi waonekana kwa mbali mjini Addis Ababa, Ethiopia, wakati wa ghasia na maandamano kufuatia kuuawa kwa mwanamuziki maarufu Haacaaluu Hundeessaa.

Watu wapatao 166 wameuawa katika eneo la Oromia nchini Ethiopia kufuatia ghasia zinazoendelea baada ya kuuawa kwa mwanamuziki maarufu nchini humo, polisi walithibitisha Jumapili.

Kifo cha Haacaaluu Hundeessaa, mwanamuziki mwenye umaarufu mkubwa anayefahamika kwa nyimbo zake za kisiasa kimeibua mivutano huko Ethiopia, huku maandamano yakisambaa kuelekea eneo la Oromia mahala ambako Hundeessaa alizaliwa.

"Raia 145 na maafisa 11 wa kulinda usalama wamepoteza maisha yao kufikia sasa," alisema Girma Gelam, naibu kamishna wa polisi katika jimbo la Oromia.

"Wengine 10 walipoteza maisha yao mjini Addis Ababa," aliongeza.

Vifo vingi vilitokea huko Oromia na wengine waliuawa katika mji mkuu wa Addis Ababa na vikosi vya usalama au katika visa vya ghasia za kikabila katika wiki iliyopita.

Kufikia sasa, angalau watu 2,000 wamekamatwa.

Maafisa wamekata huduma ya Internet katika jaribio la kusitisha maandamano na kufanya iwe vigumu kwa makundi ya haki za binadamu kufuatilia mauaji hayo, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG