Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:25

Kenya : Rais Kenyatta aondoa masharti ya kupambana na Covid-19


Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Jumatatu ametangaza kuanza tena shughuli za kawaida nchini wakati serikali ikichukua hatua ya kulegeza masharti ya COVID-19.

Rais amesema katazo la kuingia na kutoka mji mkuu wa Nairobi, na Mombasa na kaunti kadhaa za Mandera litaondolewa kuanzia saa kumi alfajiri Jumanne, na watu wataruhusiwa kuingia na kutoka katika kaunti hizi.

Hata hivyo ameongeza muda wa amri ya kutotoka nje wakati wa usiku kwamuda wa siku 30 kuanzia saa tatu usiku mpaka saa kumi alfajiri, gazeti la The East African, Kenya limeripoti.

“Tutatathmini jinsi watu wanavyokaribiana kwa siku 21 na kama kutakuwa na ongezeko la maambukizi, tutatoa amri ya kufunga shughuli nchini.

Rais pia ameruhusu kufunguliwa tena kwa sehemu za ibada, akiweka masharti ibada hizo ziwe kwa saa moja na mahudhurio yawe siyo zaidi ya watu 100 kwa wakati.

Maeneo ya ibada yatatikiwa kuheshimu masharti ya kuhakikisha usalama wa waumini wakati huu wa janga la virusi vya corona. Mafundisho ya watoto kanisani Jumapili na Madrasa za Kiislam, zitaendelea kufungwa.

Hakuna ruhusa kwa wenye umri chini ya miaka 13 au wale walio na umri zaidi ya miaka 58 kuhudhuria sehemu za ibada, Kenyatta ameongeza.

Wale wote wenye matatizo ya kiafya pia wametahadharishwa kutohudhuria mikusanyiko ya ibada.

Rais amewataka wananchi wa Kenya waendelee kushikamana na hatua za usalama za kujikinga na COVID-19 kuzuia kuenea kwa maradhi hayo.

XS
SM
MD
LG