Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:06

Rais Trump kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Marekani


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Donald Trump anatarajiwa kuchukua hatua hatarishi ya kwenda mji wa Mount Rushmore katika jimbo la South Dakota Ijumaa kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Marekani yanayofanyika mapema ambapo mamia ya watu wanategemewa kuhudhuria.

Marekani ilipata uhuru wake kutoka kwa Uingereza tarehe 4 mwezi Julai mwaka wa 1776.

Pamoja na kuwa Marekani inaongoza ulimwenguni kwa idadi ya maambukizi ya COVID-19, maafisa wa eneo hilo wanasema hakuna utaratibu wowote wa kuhakikisha watu hawakaribiani au wanavaa barakoa katika sherehe hizo. Lakini barakoa zitatolewa bure kwa wale wanaotaka kuzitumia.

South Dakota

Gavana wa South Dakota, mrepublican Kristi Noem, amesema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Fox News mapema wiki hii : “Tumewaambia watu waliokuwa na wasiwasi wanaweza kubaki nyumbani.”

Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence huko Arizona wakati wa wikiendi hii iliahirishwa kutoka Jumanne hadi Jumatano baada ya walinzi wake wanaoandaa ziara yake walikuwa wagonjwa kutokana na virusi au dalili za maambukizi.

Maambukizi mapya Marekani

Marekani Alhamisi imeripoti kuwa kuna zaidi ya maambukizi mapya 50,000. Majimbo manne – Arizona, California, Florida, Texas – wanahusika na nusu ya maambukizi hayo mapya.

Sehemu ya lawama ya kuongezeka kwa maambukizi ya COVID-19 zinaelekezwa kwa Gavana wa New Jersey Phil Murphy “ikiwa ni uzembe” – watu kutovaa barakoa au kukaidi kutokaribiana.

Kuna takriban maambukizi ya COVID-19 milioni 11 duniani. Marekani inakaribia kufikia maambukizi milioni 3.

Australia

Maafisa nchini Australia wanasema watu 10,000 huko Victoria wamekataa kupima virusi vya corona wiki iliyopita kwa sababu wanaamini kuwa milipuko hiyo siyo ya kweli na kuwa ni “nadharia za uzushi.”

Gazeti la New York Times limeripoti kuwa Australia, ambayo imekuwa na mafanikio kudhibiti maambukizi kuwa ya chini kabisa, hivi sasa inaweka amri ya kutotoka nje katika eneo lenye watu 300,000 katika jamii yenye idadi kubwa ya wakimbizi katika jimbo la Victoria.

India imeripoti takriban maambukizi mapya 21,000 kwa siku ya virusi vya corona Ijumaa.

Chuo Kikuu cha Johns Hopkins

India ilisema Alhamisi kuwa ilikuwa imerekodi kiasi cha maambukizi 100,000 katika siku nne. Chuo Kikuu cha Johns Hopkins kimesema mapema Ijumaa kuwa taifa la Asia Kusini linamaambukizi zaidi ya 625,000 ya COVID-19.

Afrika Kusini

Afrika Kusini imeripoti idadi mpya ya maambukizi mapya 8,100 katika kipindi cha saa 24 Alhamisi.

Poland

Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki amewaambia wapiga kura wasiwe na wasiwasi kujitokeza na kupiga kura zao katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais Julai 12.

Hata baada ya kuwepo mamia ya maambukizi mapya kila siku, Poland imeweza kufanikiwa kwa namna fulani kujikinga na kuenea kwa COVID-19, ikiwa na vifo 1,500.

Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema Alhamisi analegeza masharti ya karantini kwa wasafiri wanaoingia Uingereza. Amesema atatoa maelezo zaidi siku ya Ijumaa au Jumamosi.

Mexico

Na huko Mexico, kampuni inayosambaza dawa imeanza kutumia ndege ndogo zisizoendeshwa na rubani kufikisha barakoa, glovu na vifaa vingine vya hospitali.

Madaktari, wauguzi na wafanyakazi wengine wa afya wameandamana nchi nzima kupinga kile wanachosema ni ukosefu wa vifaa ya kujilinda katika kazi.

XS
SM
MD
LG