Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:19

Ubalozi wa Marekani wasikitishwa na kuminywa demokrasia Tanzania


Rais John Magufuli
Rais John Magufuli

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania imeeleza sikitiko lake katika kile walichosema ni hatua za hivi karibuni ya serikali ya Tanzania kuminya demokrasia. 

Tamko hilo limetolewa na ubalozi wa Marekani Alhamisi likielezea ni pamoja na kuwakamata viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wakiwa katika vikao vyao vya ndani na kufuta leseni ya gazeti la "chama cha siasa cha upinzani."

"Hatua hizi ni mwendelezo wa mlolongo wa matukio ya kusikitisha ya vitisho kwa wanachama wa vyama vya upinzani, asasi za kiraia na vyombo vya habari," taarifa hiyo imeeleza.

Tamko hilo limefafanua kuwa haki ya kukusanyika kwa amani na uhuru wa kujieleza ni mambo yaliyo jumuishwa na yanayolindwa na Katiba ya Tanzania na Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu.

Ubalozi huo pia umeeleza unafahari kusaidia na kuunga mkono uhuru wa kujieleza na ushiriki jumuishi wa kisiasa kwa namna zote.

XS
SM
MD
LG