Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:55

Tanzania : Mchimbaji Laizer awa bilionea baada ya kubahatika kupata Tanzanite mbili kubwa


Mchimbaji Saniniu Laizer
Mchimbaji Saniniu Laizer

Mchimbaji mmoja mdogo wa madini katika machimbo ya Tanzanite huko Arusha, Tanzania amefanikiwa kupata Tanzanite mbili kubwa zenye uzito wa kilo tisa na tano mtawalia.

Mchimbaji huyo Saniniu Laizer ambaye ni kijana wa kimasai ambaye anatokea katika jamii ya wafugaji ameishukuru serikali kwa kuchukua hatua za haraka na kuyanunua madini hayo.

Serikali ya Tanzania imeyanunua madini hayo kwa kumfanya Laizer kuwa ni miongoni mwa mabilionea wachache nchini humo. Madini hayo yana thamani ya zaidi ya shilingi bilioni saba.

Serikali imesema kupitia kwa waziri wa madini, Dotto Biteko kuwa azma ya kununua madini hayo kutoka kwa Laizer ni kuibua ari wananchi wa kawaida kuongeza bidii ya uchimbaji madini na pia kufuata sheria sambamba na kulipa kodi.

Kiongozi wa chama cha wachimbaji madini, Sam Mollel ameiomba serkali kuendelea kuwapa nafasi wachimbaji wadogo nchini Tanzania ili wajiajiri wenyewe na pia kuwa na fursa ya kujipatia kipato.

Waziri Biteko amesema ukuta uliojengwa na serikali ya Tanzania katika migodi ya madini ya Tanzanite nchini humo kwa lengo la kudhibiti utoroshaji wa rasimali hiyo umeanza kuwanufaisha wachimbaji wadogo wa madini hayo ambayo hupatikana nchini Tanzania pekee.

XS
SM
MD
LG