Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:31

Pence ashauri kuvaa barakoa baada ya ongezeko la Covid-19 Marekani


Makamu wa Rais Mike Pence
Makamu wa Rais Mike Pence

Shirika la Afya Duniani linaeleza wasiwasi wake kutokana na kuogezeka kwa maambukizo ya virusi vya corona katika baadhi ya nchi wakati idadi ya waliofariki duniani imefikia nusu milioni kutokana na janga hilo.

Marekani, India, Brazil na Russia ni baadhi ya nchi zinazoshuhudia ongezeko kubwa la wagonjwa wa COVID-19 na kuwalazimisha maafisa wa serikali kufikiria kufunga tena shughuli zote za kibiashara na watu kubaki majumbani muda mfupi baada ya kufunguliwa tena.

Wakati huohuo India na Brazil zimetangaza ongezeko kubwa la maambukizi ya virusi vya corona Jumatatu ambapo India kumekuwepo na watu 20,000 walioambukizwa na Brazil ikifikisha rikodi mpya ya watu elfu 47 walioambukizwa kwa siku moja kulingana na WHO.

Baadhi ya wilaya za jimbo la Assam nchini India zimetangaza upya masharti ya watu kutotoka nje na kufungwa shughuli zote hadi Julai 12.

Nchini Marekani, majimbo ya Florida, Texas, California na Arizona, yameshuhudia ongezeko la ghafla la maambukizo na kusababisha Makamu wa Rais Mike Pence, kuwashauri wakazi wa majimbo hayo kuvaa barakoa.

Makamu wa Rais wa Marekani

"Ikiwa maafisa wenu wa miji kwa kushauriana na wakuu wa jimbo wanakuamrisheni kuvaa barakoa , sisi tunahimiza kila mtu kuvaa barakoa katika maeneo yenye maambukizo na kujaribu kutokaribiana ikiwezekana," amesema Pence.

Pence na gavana wa jimbo la Texas Greg Abbot ambao hawakuwa wanawahimiza watu kuvaa barako walikuwa wameivaa jana walipokutana na waandishi habari na kuwalaumu vijana kutokana na kuongezeka kwa maambukizo.

Waatalamu wa afya wanaendelea kuhimiza watu kufuata masharti ya kutokaribiana na kuendelea kuvaa barakoa. Mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza Anthony Faucci ambaye ni mjumbe wa tume maalum ya White House ya kupambana na virusi vya corona, anasema njia iliyopo ni kuamua ikiwa uko upande wa kupatikana suluhisho au upande wa matatizo.

Dkt Fauchi

Dkt Anthony Fauchi anasema : "Ikiwa hatumalizi mlipuko huu basi hata wale ambao wako wazima watakuwa katika hatari ya kusambaza ugonjwa. Kwa hivyo njia pekee ya kulimaliza janga hili na kushirikiana pamoja.

Ingawa idadi ya wakazi wa Marekani ni asilimia 4 tu ya wakazi wote duniani lakini ina robo ya watu milioni 10 walioambukizwa na COVID-19. Na idadi ya wagonjwa imeongezeka kwa asilimia 25 mnamo wiki iliyopita katika majimbo ya Arkansa na Florida peke yake.

Spika Pelosi

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi anasema wakati wa kutoa amri ya kitaifa kwa watu wote kuvaa barako imefika, jambo ambalo utawala wa Trump haujatekeleza.

Spika Pelosi anaeleza : "Taasisi ya kudhibiti magonjwa imependekeza utumiaji barakoa. Lakini haikulazimisha kwa sababu haitaki kumuudhi rais. Rais ilibidi kuwa mfano mzuri. Kuwa mfano mzuri kwa nchi kwa kuvaa barakoa.

Magavana wa Texas, California wamefunga baadhi ya biashara zilizofunguliwa na Gavana wa florida anapanda kufunga maeneo yote ya pwani na Gavana wa jimbo la Washington Jay Inslee anasitisha mipango ya kuingia awamu ya nne ya kufunguliwa tena shughuli za kawaida.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG