Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:23

Rais Nkurunziza wa Burundi azikwa


Jeneza la Hayati Pierre Nkurunziza wakati wa hafla ya mazishi iliyofanyika katika mji wa Gitega, ulio katikati mwa mwa Burundi.
Jeneza la Hayati Pierre Nkurunziza wakati wa hafla ya mazishi iliyofanyika katika mji wa Gitega, ulio katikati mwa mwa Burundi.

Maelfu ya warundi walisimama kando ya barabara kuelekea mji mkuu wa Gitega, ulio eneo la katikati mwa nchi hiyo, ambako mwili wa rais wa zamani Pierre Nkurunziza ulisafirishwa chini ya ulinzi mkali kwa mazishi ya kitaifa siku ya Ijumaa.

Sala ya mazishi zilifanyika katika uwanja mkuu wa michezo wa Gitega ambako wakazi kutoka sehemu mbalimbali za nchi walikua wamevalia nguo nyeupe kutokona na wito wa maafisa wa serikali.

Katika sala hiyo, viongozi wa kidini, wakiwemo wa kanisa Katoliki na wa Kiislamu, walimuomba Mwezi Mungu "ailaze nafsi yake mahali pema na amuamehe kwa yale ambayo hakutenda akiwa kiongozi."

Nkurunziza alizikwa katika eneo lililotengwa kwa mazishi ya waathiriwa wa mizozo mbalimbali ya taifa hilo lililo katika mtaa wa Musinzira mjini hapo Gitega.

Miongoni mwa viongozi wa nchi za Afrika Mashariki waliohudhuria mazishi ya Nkurunziza ni waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, na rais wa zamani wa nchi hiyo, Jakaya Mrisho Kikwete.

Akizungumzia wasifu wa hayati rais Nkurunziza, Waziri Mkuu Majaliwa alisema kati ya majukumu makubwa aliyoyatekeleza ni kuhakikisha Burundi, Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaendelea kushirikiana katika nyanja mbali mbali.

Nkurunziza aliyetawala kwa miaka 15, alifariki ghafla tarehe 8 mwezi huu, akiwa na umri wa miaka 55 kutokana na mshituko wa moyo, kulingana na taarifa ya serikali.

Wiki jana, Rais Evariste Ndayishimiye aliapishwa kama kiongozi mpya wa taifa hilo kufuatia uchaguzi ulioibua utata.

-Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG