Mashtaka hayo yamefunguliwa baada ya kuposti video kwenye mitandao ya kijamii akiwa amefurahishwa na picha ya zamani ya Rais John Magufuli aliyekuwa amevaa suti isiyokuwa saizi yake.
Mkurugenzi wa Amnesty International eneo la Mashariki na Kusini mwa Afrika, Deprose Muchena alisema : “Mashtaka haya yamechochewa kisiasa na lazima yatupiliwe mbali mara moja.
Huu ni ‘usaliti’ kuwa Idris Sultan anafunguliwa mashtaka kwa kutumia tu uhuru wake wa kujieleza.
Kucheka siyo uhalifu. Kufanya kitendo uchekeshaji kuwa kosa la jinai ni hatua mpya kabisa ya chini nchini Tanzania katika juhudi za kukandamiza uhuru wa kujieleza.
“Ni dhahiri kuwa serikali ya Tanzania hawana kesi yoyote dhidi ya Idris Sultan na kwa uchache tu wanataka kumsumbua kwa sababu uchekeshaji wake umewakera wao binafsi. Mahakama ni lazima itupilie mbali mashtaka yaliyoletwa dhidi ya mchekeshaji huyu,” imesema Amnesty International.