Maelezo yao pia yanagusa uhamishaji wa haraka wa raia zaidi ya 124,000 ulioelezewa na Rais wa Marekani Joe Biden kama mafanikio makubwa.
Wakati wanaelezea safari ya ndege ya siku 18 kama ya kishujaa na kubwa zaidi katika historia ya Marekani, maafisa hao pia walizungumzia juu ya maumivu yao.
Wamesema wanahasira na majuto juu ya raia wa Afghanistan waliobaki nyuma, ikiwa ni pamoja na wengi ambao walikuwa wamefuzu kupata Visa Maalum ya Uhamiaji nchini Marekani.
"Naweza kusema ni wengi, afisa mwandamizi Wizara ya Mambo ya Nje aliyehusika katika operesheni ya uokoaji alisema, Jumatano, alipoulizwa ni wangapi waombaji wa visa hiyo hawakufanikiwa kuondoka.