Kundi la waasi Iran lamtaka Biden kuunga mkono harakati zao za mageuzi

Rais Joe Biden

Kundi la waasi nchini Iran, limemwandikia Rais wa Marekani, Joe Biden, kutoa mwito wa kuunga mkono juhudi za kuleta demokrasia ya kawaida na kuheshimiwa kwa haki za binadamu nchini Iran.

Inaelezwa kuwa utawala wa Rais Biden umekuwa kimya tangu hapo awali wakati unajikita katika kushughulikia mpango wa nyuklia wa taifa hilo la Kiislamu.

Katika barua ya wazi iliyo andikwa katika lugha ya Kingereza Februari 1, na wanaharakati 38 wanaoishi Marekani, kwanza wamempongeza kwa ushindi na kuanza kwa utawala wake hapo Januari 20, na kuusihi utawala wake kuunga mkono harakati zao.

Harakati zao zina malengo ya kisiasa katika kushughulikia sera za Iran.

Lengo lao kuu wameainisha ni kuhakikisha Iran inaondokana na mfumo wa sasa wa serikali na kujikita katika demokrasia ya kawaida.