Kenyatta bado hajampongeza hadharani mrithi wake

Rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta (kulia) na Rais mteule William Ruto, (kushoto) wakati akiwa naibu rais, wakizindua treni ya mizigo kwenye depot ya makoteni bandarini Mombasa, Kenya, May 30, 2017.

Viongozi hao wawili hawajaongea hadi kufikia Alhamisi, kulingana na watu wa karibu na Ruto, akiwemo naibu rais mteule Rigathi Gachagua.

Rais Kenyatta amerejea kuelezea nia yake ya dhati ya kutekeleza makabidhiano kwa utulivu, ikiwa ni uhakikisho wa karibuni katika mikutano tofauti na ujumbe wa Bunge la Marekani na kikundi cha viongozi wa kidini nchini siku ya Alhamisi.

Mipango ya kukabidhiana madaraka kwa amani kutoka kwa Rais Kenyatta kwenda kwa mrithi wake pia yanaaminika kuwa tayari yanatekelezwa – yakisimamiwa na kamati ya mpito inayoongozwa na mkuu wa huduma za umma Kenya.

Makabidhiano yanaweza kuchelewa kutokana na changamoto ya kisheria kuhusu matokeo ya uchaguzi ambayo itawalishwa na Raila Odinga.

Mahakama ya Juu nchini Kenya ilibatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais mwaka 2017, katika misingi ya kuwepo dosari katika kuwasilisha matokeo na kujumuisha kura.

Kwa mujibu wa kanuni na utamaduni wa kukabidhiana madaraka Kenya, kamati, kati ya vitu vingine, inatarajiwa kufanikisha mawasiliano kati ya rais anayeondoka madarakani na rais mteule, na rais mteule anatakiwa kupewa muhtasari wa taarifa za kijasusi.

Kenya imepitia mara tatu imekuwa na kipindi kizuri cha mpito kwa rais mpya kuingia madarakani katika miaka yake 59 ya uhuru, makabidhiano ya kwanza yalikuwa mwaka 1978 alipofariki rais Jomo Kenyatta akiwa madarakani – ambaye ni baba wa rais anayemaliza muda wake.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African" linalochapishwa Kenya